Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mzozo wa Ukraine: Kikosi cha jeshi cha Urusi kinachoogopwa kilichotumwa Crimea na kipo mashariki mwa Ukraine
Mizinga na vikosi vya Urusi vimeliweka tena katika hali ya tahadhari eneo la mashariki mwa Ukraine.
Tangu mwisho wa Machi, Kremlin imepeleka maelfu ya wanajeshi na silaha nzito katika mkoa wa Donbás, eneo lisilo na utulivu ambapo vita vya 2014 vilitokea, na kuwaacha zaidi ya watu 14,000 wakiwa wamekufa na bado kuna mzozo .
Lakini kupelekwa kwa jeshi hilo la Urusi katika eneo hilo kumesababisha pia ilani na tahadhari za majeshi ya muungano wa NATO. Moscow pia imeimarisha vikosi vyake huko Crimea, rasi ya Ukraine ambayo ilichukuliwa kwa nguvu na Urusi mwaka wa 2014.
Miongoni mwa wanajeshi wake waliotumwa katika maeneo hayo ni kikosi chenye makali na sifa kubwa.
Ni kikosi cha 56th Air Assault Brigade, ambacho kilikuwa na makao yake eneo la Volgograd takriban umbali wa kilomita 1,500
Walakini, mwishoni mwa Machi, Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu alitangaza kwamba nchi yake imepanga kukifanya kikosi hicho kuwa kikosi cha shambulio la angani na kwamba kitatumwa Feodosia, kwenye peninsula ya Ukraine.
Sio mara ya kwanza kwa Urusi kupeleka wanajeshi katika eneo ambalo imelichukua kwa lazima . Hata hivyo hali ya kukipeleka kikosi hicho kimoja ambacho kimetumika katika vita vya mara kwa mara kumesababisha hofu huko Ukraine na katika jamii ya kimataifa.
Kuwasili kwa kikosi hicho cha hewani katika eneo la Crimea kulipelekea kutolewa kwa picha nyingi za video ambapo wanajeshi wake walionekana wakiwa na bunduki na silaha kali kali wakivuka daraja ambayo Putin alikuwa amejenga kuiunganisha Urusi na Crimea .
Lakini ni nini kinachojulikana juu ya kikosi hicho na kwa nini kuwasili kwake kwenye peninsula kunaongeza wasiwasi juu ya kutumwa kwa wanajeshi wa Urusi huko?
Idadi kubwa ya wanajeshi wa Urusi
Kulingana na wataalam na waandishi wa habari wanaohudumia BBC za Ukraine na Urusi hatua ya kikosi hicho kwenda Fedosia inapaswa kuonekana katika muktadha mkubwa: ule wa uhamishaji wa zaidi ya askari 80,000 wa Urusi nje kidogo ya Ukraine katika wiki tatu zilizopita.
Vyanzo vya ujasusi vya Ukraine viliambia BBC kwamba kwa kupelekwa kwa Kikosi hicho Urusi imefikisha 16 vikundi maalum vya kijeshi katika eneo hilo vinavyojumuisha hadi wapiganaji 14,000.
Kwa jumla, kulingana na ofisi ya rais wa Ukraine , Urusi sasa ina askari wapatao 41,000 kwenye mpaka wa mashariki, pamoja na 42,000 huko Crimea.
"Labda ni uhamisho mkubwa zaidi wa kijeshi ambao Ukraine imeona katika maeneo yake ya karibu tangu 2015," Anders Åslund, mtafiti katika Baraza la Atlantiki, anaiambia BBC Mundo.
Nia ya Urusi ya kuwapeleka wanajeshi hao karibu na Ukraine haijulikani wazi, lakini wameanza kuzua wasiwasi katika mtaifa ya magharibi
Siku chache zilizopita, afisa mwandamizi wa Urusi alitoa hakikisho kuwa nchi yake inaweza kuingilia kati kuwatetea watu wanaozungumza Kirusi mashariki mwa Ukraine, na akasema kuwa kuongezeka kwa mzozo kunaweza kuwa "mwanzo wa mwisho kwa Ukraine."
Dmitry Kozak alilinganisha hali ya Warusi wanaotaka kujitenga na ile ya Srebrenica, jiji la Bosnia na Herzegovina ambapo wanaume 8,000 Waislamu waliuawa na vikosi vya Waserbia wa Bosnia mnamo 1995.
Rais Biden alisisitiza kujitolea bila kutetereka kwa Marekani kwa uhuru wa eneo la Ukraine," ikulu ya White House ilisema katika taarifa.
Tume ya NATO pia ilikutana mjini Brussels Jumanne kujadili hali katika eneo la Donbas na Crimea, ikitoa wito kwa Urusi isimamishe mkusanyiko wa wanajeshi wake katika eneo hilo.
Kikosi hicho katika vita vya hivi karibuni
Kulingana na data kutoka kwa Wizara ya Ulinzi ya Urusi, kikosi hicho cha Brigade 56 kiliundwa mnamo 1946 kutoka kwa vikosi viwili vidogo ambayo moja ilikuwa imepigana huko Hungary kama kwa upande wa Ukraine
Katika miaka ya 1980, kilikuwa moja ya vikosi vya Urusi kwenye vita vya Afghanistan na baadaye katika vita viwili vya Chechen (kwanza mnamo 1994 na kisha 1999).
"Sehemu ya kikosi hicho ndiyo iliyotumwa katika mpaka na Georgia huko Chechnya," Shramovich anaelezea.
Kikosi hicho pia kilifanya oparesheni za ardhi ni na kilitekeleza kile kinachoitwa "mafundisho ya Grozny", ambayo yalikuwa na upangaji wa mabomu katika mji mkuu wa Chechen na kisha kuwezesha kuingia kwa wanajeshi na silaha nzito.
Baada ya Vita vya Pili vya Chechen, kikosi hicho kilikuwa kimewekwa katika jiji la Kamyshin, katika mkoa wa Volgograd.
Mafunzo ya hali ya juu
Mykola Beleskov, mshauri mkuu wa Taasisi ya Kitaifa ya Mafunzo ya Mkakati huko Ukraine, anasema kuwa moja ya sifa za kikosi hiki ni mafunzo yake ya kiwango cha juu na kupelekwa kwake katika maeneo ambayo Urusi ina masilahi ya kuanzisha mzozo.
"Hiki ni kikosi kinachoshiriki kikamilifu katika mazoezi ya kiwango cha juu. Jeshi lote la Urusi linapata mafunzo ya kiwango cha juu sana, lakini katika wapiganaji hawa mafunzo huenda hatua moja zaidi," aliiambia huduma ya BBC ya Ukraine
Wanaandaa wanajeshi na makamanda wao kuchukua hatua kwa kina juu ya ulinzi wa adui, kukamata uongozi wa vikosi pinzani na kupenyeza katika ngome za mahasimu wao kutokea pembeni au kutoka nyuma," anaongeza.