Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Simba kucheza bila ya mashabiki Dar es Salaam
Klabu ya Simba SC ya Tanzania itacheza mchezo wake wa ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Al Merrikh bila ya mashabiki kuhudhuria mchezo huo utakaochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumanne, Machi 16.
Msemaji wa klabu ya Simba Haji manara amewaambia waandishi habari "Mechi yetu na Al Merrikh ipo pale pale lakini wakati tukiendelea na maandalizi tumepokea taarifa kutoka TFF ambayo imetolewa na CAF kwamba tucheze bila mashabiki."- Haji Manara.
Msemaji huyo akaongezea kwa kusema "Simba imezoea kucheza bila mashabiki ikiwa nje ya nchi lakini sikumbuki kama hapa nchini tumewahi kucheza bila mashabiki. Tunawaomba radhi mashabiki kwa mechi hii sababu ni maamuzi ya CAF ambao ndio wenye mamlaka ya soka Afrika."- Haji.
Kuna uwezekano mkubwa wa michezo yote ijayo ya ligi ya mabingwa na ile ya Kombe la shirikisho kuchezwa bila mashabiki.