Uganda yachunguza idadi kubwa ya vifo vya samaki ziwa victoria

National Environment Management Authority

Chanzo cha picha, National Environment Management Authority

Maelezo ya picha, Mamlaka ya mazingira ya Uganda yachunguza vifo vya samaki

Mamlaka ya Uganda inachunguza idadi kubwa ya vifo vya samaki katika ziwa victoria, ambalo ni ziwa kubwa barani Afrika.

Wizara ya uvuvi nchini Uganda imetoa onyo kwa umma kutokula samaki waliokufa na wanapaswa kuwazika.

Haijafahamika bado ni kiasi gani cha samaki ndio wameathirika.

Lakini picha katika mitandao ya kijamii zinaonesha samaki wengi wakiwa wamekufa katika fukwe za ziwa victoria.

Samaki wanaoweza kukua mpaka kufika zaidi ya kilogramu 100, na ndio chakula kikuu nchini Uganda ndio wameathirika.

Taarifa kutoka mamlaka ya mazingira ya taifa inasema inawezekana vifo hivyo vimetokana na kukosekana kwa kiwango cha kutosha cha oksijeni.

Samaki hao wanadaiwa kuwa katika kiwango cha chini cha oksijeni katika lia moja ya maji.

Uchunguzi zaidi unaendelea, kwa mujibu wa mamlaka.

Ziwa victoria lipo Uganda, Kenya na Tanzania.