Marais Uhuru kenyatta wa kenya na mwenzake wa Somali Mohamed Farmajo wakutana ana kwa ana mkutano wa IGAD

Kulingana na picha zilizochapishwa na Ikulu ya rais nchini Kenya siku ya Jumapili, December 20 , viongozi hao wawili walionekana katika mkutano ambao pia ulihudhuriwa na waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed na mwenzake wa Sudan Abdalla Hamdok.
Menyekiti wa muungano wa Afrika Moussa Faki Mahamat, ambaye alikuwa mmoja ya wazungumzaji katika mkutano huo alizungumzia kuhusu umuhimu wa kutatua mgogoro kati ya Kenya na Somalia.
''Hali ya wasiwasi ilioshuhudiwa hivi karibuni kati ya Kenya na Somalia inatutia wasiwasi katika muungano huu . Hivyobasi , ningependa kuomba mataifa yote mawili kuanza mazungumzo ili kurudisha uhusiano wa kidiplomasia na ningependekeza IGAD kuunga mkono pendekezo hili'', alisema Moussa.
Taifa la Somalia limekatiza rasmi uhusiano wa kidiplomasia na Kenya huku taifa hilo likiendelea kuilaumu Kenya kwa kujaribu kuingilia uhuru wa taifa hilo kujitawala.
Kenya ilitakiwa kuwaondoa maafisa wake wote wa kidiplomasia nchini Somalia chini ya kipindi cha siku saba huku taifa hilo pia likiwaondoa wanadiplomasia wake nchini Kenya.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Awali balozi wa Kenya nchini Lucas Tumbo aliagizwa kuondoka nchini humo kwa mashuariano zaidi japo hatua hii ya hivi punde sasa inamaanisha hatarejea kamwe hadi masuala tata yatatuliwe
Mkutano huo wa IGAD uliongozwa na waziri mkuu Abdalla Hamdok wa Sudan ambaye ni mwenyekiti wa mkutano wa IGAD na kuhudhuriwa na rais Ismail Omar Guelleh (Djibouti), Mohamed Abdullahi (Somalia) na waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed.
Katika mkutano huo ambao ulihudhuriwa pia na mwenyekiti wa tume ya umoja wa Afrika-African Union Commission (AUC) Moussa Faki Mahamat, makamu wa rais wa Sudan Kusini na Uganda Rebecca Garang na Amb Rebecca Otengo.

Chanzo cha picha, Ikulku ya rais kenya/Twitter
Katika utangulizi ,mwenyeji wa mkutano huo rais Ismail Guelleh alipongeza jitihada zinazofanyika katika kutafuta amani na utulivu katika ukanda huo licha ya janga la corona na changamoto nyingine za mafuriko pamoja na jangwa la ukame lililosababishwa na uvamizi wa nzige.
Katika hotuba yake, mwenyekiti wa AUC bwana Moussa Faki Mahamat alisema mvutano wa kidiplomasia kati ya Kenya na Somalia ni suala ambalo Umoja wa Afrika una wasiwasi nao.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Bwana Mahamat aliitisha mazungumzo haya ili mvutano huo wa mataifa majirani ambayo yana historia ya uhusiano mzuri kwa muda mrefu , kwa mfano Kenya imejitoa pakubwa kutoa wanajeshi wake katika jumuiya ya Afrika nchini Somalia (AMISOM) na kusaidia kupokea wakimbizi wengi wa Somalia .

Chanzo cha picha, Ikulu ya rais Kenya/twitter
Kwa upande wa Ethiopia,mwenyekiti wa AUC iliwataka wanachama wa IGAD kusaidia taifa hilo kwa misaada ya kibinadamu kufuatia ghasia zilizokuepo Tigray.
Waziri mkuu Hamdok alisema mkutano huo uliitishwa ili kujadili masuala mbalimbali ya amani katika ukanda huo katika upande wa amani na usalama wa Sudan, Sudan Kusini , Ethiopia na Somalia.
Rais Kenyatta, ambaye aliwasili Djibouti Jumapili asubuhi aliongozana na waziri wa mambo ya nje Raychelle Omamo.












