Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
"Mara ya kwanza kugundua kuwa korodani zangu zina matatizo nilikuwa na miaka 15"
Inawezekana kuna watu wengi ambao hawajui jinsi ya kutunza korodani zao au kujua namna zinavyofanya kazi?
Ni swali ambalo katika kipindi cha uhalisia cha Uingereza na mshiriki mmoja Chris Hughes alijiuliza mwenyewe, na kwa zaidi ya miaka miwili iliyopita, wakati anasumbuka na korodani zake.
Chris, 27,na kaka yake Ben, 28, walionekana kwenye Makala ya BBC Three iitwayo 'My, my brother and our balls ' ambako walikuwa wanachunguza afya za korodani zao ili kuwahamasisha watu wengine kufanya vivyo hvyo.
"Nilifanya upasuaji mara nne wa korodani zangu na mara ya kwanza kugundua kuwa nina matatizo katika korodani zangu nilikuwa na miaka 15 hivi. " Chris alieleza.
"Nilikuwa sisumbuki sana, hivyo kwa miaka michache sikufanya chochote.
Sikuliwekea akilini suala hilo.
Lakini baada ya miaka michache, ilinibidi nifanye upasuaji upande wa kulia wa korodani."
Mwaka 2018, Chris alifanya vipimo wakati kipindi cha televisheni kikiwa kinarusha matangazo yake mubashara.
Lakini anasema hakuwa huru na mchakato wote ambao alikutana nao wakati wa siku za nyuma katika korodani zake.
Hatahivyo hakujua au kuwaza athari ambazo kaka yake angekutana nazo.
"Alirudi nyumbani saa 1:00 asubuhi na nilimpongeza,nilimwambia alichokifanya kitaenda kuwasaidia watu wengi , bila kujua kuwa ataisaidia mimi pia.."
Ni pigo kubwa
Usiku ule, nilihamasika kwa kile ambacho kaka yangu alikifanya, Ben aliamua kufanya vipimo pia kujua hali ya korodani zake na kukuta pia zina tatizo.
"Ilikuwa kama bahati tu kuwa Chris alifanya vipimo wakati televisheni ikimuonyesha na mimi pia nikagundua nina tatizo katika korodani zangu."
"Sikuwahi kuwaza kitu kama hicho kabla, hatusikii au kuona matatizo ya korodani kuongelewa katika mitandao ya kijamii au TV, na imeona katika namna ya kushangaza sana."
Baada ya kufanya vipimo, walithibitisha kuwa korodani zangu zina tatizo kubwa.
Lakini kabla halijaondolewa, Ben aliamua kuondoa baadhi ya mbegu zake za kiume, kama atahitaji kupata watoto kwa siku za usoni.
Baadae akapata pigo lingine
"Kiwango cha kuzalisha mbegu kilikuwa chini . Hivyo wakanisafirisha mpaka London na kukutana na madaktari wengine.
Walinipa tiba ya miezi miwili baada ya upasuaji," alisema.
Tangu uvimbe uondolewa katika korodani yangu mwezi Januari 2019, Ben amekuwa anajaribu kufuatia sababu inayosababisha matatizo yake ya mfumo wa uzazi.
Yeye na mpenzi wake Olivia,hawajaanza kutafuti watoto kwa sasa lakini wangependa kuwa nao siku za usoni.