'Black Lives Matter': 'Ni jukumu langu kama mzazi kumwambia kuhusu ubaguzi'

Kuungwa mkono kwa vuguvugu za harakati za mtu mweusi 'Black Lives Matter' kuenea nchini Uingereza tangu kuuliwa kwa George Floyd, tukio hilo limesababisha wazazi wengi kupata wakati mgumu kuwafafanunulia watoto wao kuhusu ubaguzi wa rangi.

"Kwa nini wanasema hivyo?" swali la Denis Adide, mwenye umri wa miaka mitano alimuuliza baba yake wakati akihoji kuhusu bango lililoandikwa 'Black Lives Matter'.

"Huu ni uhalisia kwa watoto weusi, huu ni uhalisia kwa baba wa watoto weusi," Denis alisema. "Huwezi kuishi maisha ya kifahari na haki kama watu wengine wanavyoishi."

"Ninafahamu kuwa kuna watoto wengine ambao wanahusika katika historia ya watu weusi kwa mara ya kwanza katika maisha yao," alisema.

Alisema hayo wakati watoto wake watatu , ambao wote wako chini ya miaka mitano hivyo ni wadogo kuweza kuelewa moja kwa moja kuhusu kile kilichomtokea George Floyd, anafahamu kuwa kuna wazazi wengine pia wameathirika katika hilo.

Alitoa mfano wa binti wa rafiki yake , ambaye alibaki na machozi na kubaki kustaajabu kama yuko salama kwa sababu rangi yake ni nyeusi alihoji kama anapaswa kuwa na wasiwasi wa usalama wa maisha yake.

"Ni kama jambo jipya lililowaamsha watoto, walikuwa hawalifahamu - lakini linawachanganya na linawaumiza sana kwa sababu wanaona linawahusu moja kwa moja katika mwili wao.

Si rahisi kukana mwili wako sasa hofu yao ni namna gani janga hili wanaweza kuliepuka."

Denis, kutoka Magharibi mwa London, anasema kuwafundisha watoto wake namna ya kukua Uingereza wakiwa na ngozi nyeusi ni sehemu ya kazi yake.

Anasema amekuwa akisimamishwa mara nyingi na polisi na kutafutwa na polisi, akiwa mtu mzima na wakati akiwa mtoto na inasikitisha kuwa inabidi amuandae mtoto wake mwenye miaka minne, anaweza kutendewa kama yale ambayo amekuwa akiyapitia.

Anatarajia kuwa na mazungumzo tofauti na binti yake, haswa katika upande wa muonekano wake katika jamii.

Binti yake mkubwa

Binti yake mkubwa "alifurahi ghafla", anasema, wakati alipokuwa anafundishwa siku moja na mwalimu wa mazoezi kwenye shule ambayo pia alikuwa mchanganyiko wa asili ya watu. Alimwambia baba yake, bila kusita, "leo mwalimu alikuwa na nywele kama zangu, na ngozi iliyofanana na yangu".

Georgena Clarke kutoka Cheshire anasema alikutana na changamoto inayofanana hivyo kutoka kwa watoto wake mapacha wenye miaka saba, wakiume na kike.

Suala la rangi ya ngozi liliibuliwa na binti yake. Alisema

Anasema aliona utofauti wake na watu wengine katika mtaa wake na kwa kuwa aliwaona kwa uchache sana alihisi kila mtu mweusi alikuwa na uhusiano nao".

Alikuwa ni mtoto mweusi pekee darasni na siku moja alikataa kutoka katika gari lao alipofika shuleni na kusema mama, sitaki kwenda kwa sababu ni mimi tu ndio niko tofauti".

"Nilibaki na mshangao tu ,"alisema Georgena. "Sikujua ninaweza kusema nini kwa wakati ule na nilifahamu kuwa sijafanya kazi yangu ya kumuelimisha zaidi kuhusu uasili wake.

"Awali nilikuwa ninamwambia kuwa yeye ni wakipekee, ni yeye tu ndio ana macho ya kahawia na una muonekano tofauti na wengine wote, lakini jibu hilo halikumridhisha ."

Georgena alimfafanulia binti yake kuwa wazazi wa mama yake walikuwa waafrika na wazazi wa baba yake walikuwa wametokea magharibi ya India na nchi hizo watu wanafanana na sisi.

Hivyo alitumia mtando wa YouTube ili kumuonyesha video za kuthibitisha kile ambacho anakisema.

"Sikuwahi kumuona mtu ambaye anachukulia umakini suala nililomwambia kama yeye na kila mtu aliyekutana naye alikuwa anamwambia alipotoka. Alikuwa anajivunia sana muonekano wake."

Georgena anasema anakubali kuwa haki yao wataipata tu wakati fulani, ingawa anatamani wabaki watoto kadri inavyowezekana.

"Nataka wajivunie ukweli kuwa wao ni watu weusi na kutohisi kuwa utofauti wao ni kitu kibaya," alisema.

"Kama nitawaambia kuhusu ubaguzi, na kuwaleta katika dunia yao kwa sababu ya utofauti wao, jambo hilo litaathiri kujiamini kwao."

Huko Hackney, mashariki mwa London, Marvyn Harrison ambaye ni baba wa watoto wawili ana wasiwasi kuhusu mtoto wake wa kiume mwenye miaka minne atakavyopokelewa shule .

"Mtoto wangu anajiamini sana. Hii ni changamoto kubwa kwa wanaume weusi. Kwa uelewa wangu katika suala ya kujiamini linavyofanana kwa mtu ambaye sio mweusi, suala la kuambiwa kuhusu rangi yake kunaweza kumnyima raha na kuona kama mzigo mzito unaomzidi nguvu au kuona anadhalilishwa."

Anasema anajaribu kumfundishaa mwanae utofauti wa wa tabia wakati atakapoanza masomo katika shule mpya.

Wanatembea katika maisha yao ya nyuma katika kila siku za maisha yao, alinyamaza kidogo kwa dakika chache wakati anamsimulia mwanae kuhusu kile kilicho mbele yake ambacho ategemee kukutana nacho.

'Ninapenda nywele zangu, ninapenda ngozi yangu'

Marvyn, ambaye alikutana na kundi la baba weusi mtandaoni alikuwa na hofu ya kile kilichomtokea akiwa shuleni , kuwa na rangi nyeusi kuna maanisha kuwa inabidi utengwe au walimu kumuhudumia tofauti na wengine na kupata ujumbe kuwa mtu mweusi ni uko katika maisha duni.

"Mara nyingi kile kinachowatokea watoto weusi ni kuhoji kwa nini anachukuliwa tofauti na wengine - Ninahisi kuwa nipo sawa kabisa na Sue ambaye anakaa karibu nami laikini mimi ndio niko katika wakati mgumu zaidi ya wengine'. Hivyo unaanza kuishi ukiwa unadhani kuhoji kwa nini na kuanza hata kushuka katika masomo."

Anataka watoto wake wafahamu kuw akuwa na rangi nyeusi sio jambo baya na kila siku anamfundisha kujikubali.

"Anajiangalia kwenye kioo na kusema 'Ninapenda nywele zangu, Ninapenda ngozi yangu, Ninapenda kucheza kwa kurukaruka na kukimbia, Mimi ni mkarimu'. Anasema maneno hayo kila siku ili yakae kichani mwake hata kama mtu akija kumkebei kwa rangi yake aisiweze kutetereka."

"Ni muhimu kumuandaa mapema uwezavyo - unabidi ufanye hivyo kadri unavyoelewa."

Jinsi ya kuongea na watoto kuhusu ubaguzi

Dondoo kutoka shirika la kimataifa linaloshughulikia watoto, UNICEF:

Watoto wenye umri chini ya miaka mitano:

  • Inabidi utumie lugha ambayo ni sahihi au ataielewa mtoto wa umri huo.Eleza suala la kupatana na kusheherekea utofauti
  • Kuwa muwazi - kuwa muwazi wakati unajibu maswali ya mwanao. Kama wanaainisha kuwa watu wako tofauti katika muonekano wao , usieleze mambo ya utamaduni wa kusadikika bali ukweli tu.
  • Kuwa na usawa katika kueleza mambo - tumia mbinu ya kumueleza mifano ambayo mtoto wa miaka mitano anaweza kuelewa kwa urahisi na vizuri. Zungumzia kuhusu ubaguzi bila kuegemea upande wowote.

Miaka sita mpaka 11 :

  • Hawa huwa wanapata fursa ya kupata taarifa nyingi hivyo inaweza kuwa ngumu kuelewa. Inabidi kuwa mdadisi. Hatua ya kwanza ni kusikiliza na kuuuliza maswali
  • Jadili kile kilichozungumzwa kwenye vyombo vya habari au mitandao kwa pamoja, mtoto wako anaweza kuwa chanzo chako cha habari
  • Ongea kwa uwazi - kuwa mkweli na jadili kwa uwazi kuhusu ubaguzi na kujenga kuaminiwa. Itamuhamasisha kukuuliza maswali na kusema hofu zake.

Miaka 12 na kuendelea:

  • Vijana wana uwezo wa kuelewa na kuchuja mambo na kuelezea mawazo yao. Tafuta namna ya kkufahamu nini wanakifahamu. Nini wamekisikia kwenye taarifa za habari, kutoka shuleni na kwa marafiki zao.
  • Uliza maswali kuhusu jinsi wanavyochukulia suala hilo au tukio hilo na anza kufafanua kwa mtazamo mwingine ili kumsaidia aelewe zaidi jambo hilo.
  • Msisitize kuchukua hatua