Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kifo cha George Floyd: Mizizi ya ubaguzi inapandikizwa tangu utotoni
Marekani ikiwa katika ghasia za maandamano baada ya nchi kushindwa kukabiliana na changamoto ya ubaguzi kwa karne kadhaa.
Maelfu kumi ya watu wameandamana katika miji zaidi ya 75 nchini Marekani kuandamana dhidi ya kifo cha George Floyd, Mmarekani mweusi aliyefariki Mei 25 , mjini Minneapolis wakati afisa polisi alipokuwa akiendelea kushindilia goti lake shingoni wakati mtu huyo akisisitiza kusema hawezi kupumua.
Maandamano sasa yameongezeka katika miji ya mataifa mengine ikiwemo London, Berlin na Auckland pamoja na kwenye mitandao ya kijamii ambayo imekuwa ikiunga mkono ujumbe wa Juni 2, Jumanne nyeusi'#BlackoutTuesday'.
Maandamano ya sasa ni matokeo ya mazingira ya sisi watu weupe tulikuwa tumetengeneza , tunaona athari ya tabia zetu ambazo tulitengeneza," Jane Elliott mwenye miaka 87, mhamasishaji wa kampeni ya kupinga ubaguzi aliiambia BBC, "huwezi kuwanyanyasa watu kwa miaka 300 na utarajie kuwa watavumilia milele."
Baadhi ya maandamano yanajumuisha au kulinganishwa na kampeni za Aprili 4, 1968, wakati ambapo Martin Luther King Jr alipokuwa akifanya kampeni za haki ya mtu mweusi.
Elliott alipoibuka akiwa binti mdogo :alianza kufanya kampeni kwa mifano ya vitendo ili kuwafanya watu wakabiliane na tabia yao ya ubaguzi ambayo haina huruma s, baadae akajulikana kama mkufuzi na mhamasishaji dhidi ya vitendo vya kibaguzi.
Macho ya bluu, macho ya kahawia
Elliott alitaka watu wafahamu na kuelewa namna ubaguzi unavyochukuliwa kuwa jambao la kawaida katika jamii.
Wakati Martin Luther King Jr alipouwawa, Elliott alikuwa mwalimu mdogo katika shule moja ya jimbo la kati katika kijiji cha Iowa. Siku iliyofuata , alienda kazini na kuweka zoezi kubwa la kuwafundisha wanafunzi wake kuhusu ubaguzi ni nini na athari zinazoweza kutokea kutokana na ubaguzi.
Aliweka swali hilo au zoezi kwa kuliita "macho bluu, macho kahawia" - rahisi kabisa kwa watoto wadogo kuelewa na tatizo linaloweza kusababishwa , pale mmoja anapojifanya kuwa mshupavu zaidi ya mwingine kwa sababu ya rangi ya ngozi yake.
Elliott aligawa darasa lake kwa makundi mawili: Kundi la kwanza aliwapa kitambaa cha rangi ya kahawia na kuwaambia kuwakilisha "Macho ya brown"; Kundi lingine linalowakilisha kundi la "Blue Eye"
Baadae akawaambia darasa zima kundi la "Brown Eyes" ndio walikuwa werevu zaidina wasafi , na akawapa upendeleo wa kucheza muda mwingi zaidi.
Elliott alisema pia watoto wa "blue-eyed" walikosea kila kitu, hivyo kama wanataka kunywa maji sawa na watoto wenye macho ya kahawia, inabidi watumie vikombe vile vya kutumia mara moja ili wasipate maambukizi.
Elliott alisema mabadiliko ya tabia ni kitu ambacho watu wanajengewa: watoto wa kundi la "Macho kahawia" walipata ujasiri zaidi, hawakuwaonea huruma watoto wa kundi la macho ya bluu.
Jumatatu iliyofuata, Elliott alirudia zoezi hilo lakini wakati huu alibadilisha majukumumu yao.
Mwishoni mwa zoezi hilo , aliwauliza watoe maoni yao kwa kile ambacho wamekipitia.
"Wale waliokuwa katika kundi la macho ya kahawia walijitenga na wale wa macho ya bluu," alisema binti mmoja aitwae Debbie Hughes, maelezo yake katika mtandao wa taasisi ya Smithsonian alisema, "Nilikuwa na macho ya kahawia na niilihisi kama kuyapiga kama ningetaka."
Wapo wengi ambao wanakubaliana na maoni ya Debbie.
Lakini alipobadilishiwa majukumu, nilihisi kama nataka kuacha shule. Nilikasirika . Hii hali ndio huwa inatokea unapobaguliwa".
Elliott aliliita zaoezi hili kuwa sindano ya kirusi hai cha ubaguzi".
Zoezi la "Blue Eyes, Brown Eyes" baadae lilipata umaarufu kimataifa kwa miaka mingi , maelfu ya watu duniani huwa unashiriki kampeni hiyo.
Mwaka 2016, Elliott alitajwa kuwa miongoni mwa wanawake 100 wa BBC , katika mradi wa wanawake unaoangalia shughuli walizofanya kwa karne ya 21.
Lakini zoezi lile lilishindwa kueleweka hapo baadae, kuna walioita kuwa zoezi la "Orwellian" (baada ya maelezo ya wazo la George Orwell ambayo yanalenga ustawi wa uhuru wa waztu na jamii ya uwazi) hii ikiwa inafundisha kujichukia na mwandishi Denver aliita kuwa ni uovu wa kishetani.
Swali rahisi
Lakini Elliott amefanya kazi kubwa na watu wazima pia.
Mfano mmoja wa Elliott ulirekodiwa katika makala ya mwaka 1996 ya "Blue Eyes," ambayo ilichukua jina la zzoezi ambalo alikuwa amelitaja.
Elliott alitoa ombi kwa watu wote kwenye ukumbi "Ninataka watu wote weupe kwenye chumba hiki wasimame, kama utafurahia kufanyiwa kile ambacho watu weusi wanafanyiwa katika jamii".
Palikuwa na ukimya wa ajabu uliofuata, kila mtu alimuangalia Elliott akiwa amekaa.
" Mlinielewa?" Elliott alisisitiza. "kama mnataka kufanyiwa sawa namna watu weusi wamekuwa wakiwa wakifanyiwa katika jamii, tafadhali simama juu".
"Hakuna aliyesimama," Elliott alikaa kimya kwa sekunde kadhaa.
"Hii inaonyesha wazi kuwa kile kinachoendelea , mnakifahamu na hamtaki kiwatokee nyinyi
Na kwa nini unaruhu watu wengine iwatokee?" aliuliza.
Taarifa zaidi kuhusu kifo cha Floyd:
- Mwanamichezo, rafiki na baba - George Floyd alikuwa nani?
- Sababu 3 zinazoonesha watu weusi hubaguliwa Marekani
- Tunafahamu nini kuhusu maafisa 4 wa polisi waliohusishwa na kifo cha George Floyd?
- Maandamano yaendelea usiku kucha Marekani kufuatia kifo cha George Floyd
- Ulimwengu unasema nini kuhusu maandamano Marekani?
Elliott aliiambia BBC kuwa anaamini watu hawajaribu kuchukua hatua dhidi ya ubaguzi kwa watu weusi kwa kuwa kama wangekuwa wanajua ubaya wake wasingependa hali hiyo iendelee na wangekuwa na hofu je ikitokea kwao itakuwaje?
"Watu weupe wanafahamu kuwa ni kitu ambacho wanapaswa kuwa na hofu nacho.
Hawataki kunyanyuka na je wakifanyiwa hivyo wao hali itakuwaje."
Ni rangi tu
Elliott anasema zoezi yanatolewa kuonyesha mfano rahisi wa namna ubaguzi ni kitu ambacho kinapandikizwa kuanzia utoto
"Kila mtu mweupe anayezaliwa na kukulia Marekani na sio mbaguzi ni maajabu," alisema.
"Ubaguzi ni tabia ambayo watu wanajifunza. Hakuna mtu anayezaliwa akiwa anajiona kuwa bora zaidi ya mtu mwingine.
Tabia hiyo ya kujiona kuwa bora zaidi ya mwingine huwa inafundishwa na ndio tunawafundisha nchini kwetu," alisema Elliott.
Kwa mujibu wake, mfumo wa elimu ya Marekani umebuniwa kuwaona kuwa watu weupe ndio wako juu ya watu weusi.
Lakini katika hali hiyohiyo, ubaguzi unatengenezwa na unaweza kuondolewa. Watu wanaweza kufundishwa kuacha kuwa wabaguzi, alisema Elliot.
"Macho ya watu na rangi za ngozi zisiwe sababu ya kuhukumu watu .