Wapenzi wasioona waliofunga pingu za maisha wasimulia safari yao ya mapenzi

Imezoeleka kusemwa mapenzi ni upofu, lakini inakuwaje pale ambapo walemavu wa macho wanapopendana?

"Kuna namna ya kipekee ya mapenzi ambayo mtu unaweza kupata; Mapenzi ambayo hayahusishi uzuri wa muonekano mtu; mapenzi yaliyo zaidi ya muonekano," alisema mpiga picha mahiri nchini India ndugu Niraj Gera.

Katika mfululizo wa picha alizopiga hivi karibuni alizoziita mapenzi yaliyounganishwa na Mungu, alieleza simulizi ya wapenzi wawili ambo ni walemavu wa macho kwa kutumia picha 13.

"Nilikuwa nafanya manunuzi katika maduka makubwa mjini Delhi, siku ya mwisho wa mwezi wa Julai wakati nilipowaona wapenzi waliokuwa wanapendeza kwa pamoja .

Walikuwa wanatembea huku wameshikana mikono, walikuwa wanatabasamu huku wakiwa wanaongea," Bwana Gera aliiambia BBC.

Wapenzi hawa walikuwa wanasaidiwa na mwanaume mmoja ambaye alikuwa alikuwa anawaongoza.

Bwana Gera aliseama kuwa alivutiwa kuwaona: "Ilikuwa mara yangu ya kwanza kuona wapenzi ambao ni walemavu wa macho wote."

Aliwasogelea na kuomba kuwaongoza.

"Nikiwa njiani, nilianza kuongea nao na kuwauliza kama wao ni wapenzi na kusema kuwa ndio.

Hivyo niliwauliza kama watapenda kusimulia stori yao ya mapenzi wakasema ndio." alisema.

Stori ya mapenzi yaliyounganishwa na Mungu ya Deepak Yadav na Arti Chaurasia, ambao wote wana miaka 21 walikutana kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook.

Deepak alisema kuwa wote wawili wana simu aina ya smartphone ambazo zina programu kwa watu ambao hawawezi kuona.

Siku moja mwezi June 2018, Deepak alisema kuwa jina la Arti' lilikuja katika mapendekezo la marafiki.

"Nilidhani kuwa tuna mambo mengi ambayo yanafanana hivyo nkamuomba urafiki," aliiambia BBC.

Arti alitumia wiki mbili kujibu. "Nilikuwa simjui hivyo nilikuwa bado ninashangaa huyo ni nani?" alisema. Lakini baadae akamkubali urafiki.

Na kuanza kutumiana ujumbe mfupi, na kuanza kusimuliana stori za kila mmoja na mwishoni kubadilishana namba za simu.

"Tulizungumza kwenye simu Julai, 31," alisema Deepak. "Tuliongea wa muda wa dakika 90," aliongeza Arti.

Walianza kuongea tena kila mara na siku moja, Arti alimuuliza kama anaweza kuwa mpenzi wake.

"Alisema hapana," akicheka.

Lakini haikumchukua muda mpaka kukiri mapenzi yake kwake.Waianza kuwa wapenzi Agosti 10.

"Tuliongea jana kwenye simu. Nilikuwa nimekaa karibu na rafiki yangu na alithubutu kuniambia kuwa ananipenda na mimi pia nikamwambia kuwa ninampenda pia," alisema Arti.

Deepak alisema kuwa alibaki kuwa kimya kwa dakika moja. "Nilidhani kuwa hii ilikuwa upande wangu. Amewezaje kusema hayo? Nilikuwa kimya kwa muda mdogo na kumwambia pia ninampenda."

Miezi miwili baadae, Deepak alienda kwa bweni na wapenzi hao walikutana kwa mara ya kwanza.

Tangu wakati huo, Deepak na Arti wamekuwa wakikutana mara kwa mara, na mahusiano yao yalizidi kukua.

Deepak alisema kuwa waliweza kuweka uhusiano wao wa mapenzi kuwa siri kwa familia yao kwa sababu walikuwa watu wagumu kuelewa.

"Baba yangu aliniambie niepuke na mapenzi kwa sasa, kuna muda mwingi hapo baadae.

Sasa hivi napaswa kuzingatia kwenye masomo yangu na kutengeneza maisha yangu ya baadae," alisema.

Arti alisema kuwa ndugu zake wengi wanafahamu kuhusu mahusiano yake na Deepak, Ingawa baba yake hajaridhia yeye kuwa katika mahusiano, niliuliza kama ripoti ikitoka BBC na wazazi wao wakabaini mahusiano yao nini kinaweza kutokea.

" Tunatamani waseme kuwa wanakubali mahusiano yetu," alisema Deepak.

"Kama wakisifia mahusiano yetu, nadhani wataridhia mapenzi yetu pia," aliongeza Arti.

Kwa sasa wapenzi hawa wanatafuta ajira kwa ajili ya kujikimu katika maisha yao ya baadae pamoja.

"Nitamchumbia punde mara baada ya kupata ajira," alisema Arti. "Lakini mara nyingine tuna hofu kuwa kama tukipata kazi wakati miaka imeenda, itakuwa ngumu kwao kuishi vizuri katika ndoa.."

Photographs: Niraj Gera