Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Hewa chafu Kenya: Namna kampeni ya wahamasishaji inavyosaidia kupambana na hewa chafu
- Author, Solomon Serwanjja
- Nafasi, BBC News Komla Dumor award winner 2019
Mara zote John Kieti amekuwa akihakikisha kuwa madirisha yake yamefungwa na mapazia zote nyumbani kwake zimefungwa.
Alifanya hivyo ili kuzuia hewa chafu inayotoka mji wajirani kuingia ndani ya nyumba yake.
Hewa chafu imekuwa ikiwaathiri watoto wake wawili.
''Tumeamua kuwa imetosha sasa. Hatuwezi kuendelea kuvumilia tena,'' aliiambia BBC.
''Kila siku , tunaamka na kuvuta hewa yenye vumbi . Watoto maeneo haya wanasumbuliwa sana na kupumua''
Syokimau ni mji wenye uchumi wa wastani uliopo aribu na Nairobi, mji huo una makazi ya watu zaidi ya 5,000, wengi wao wakiishi katika nyumba za vyumba viwili au vitatu.
Lakini kuna viwanda kadhaa sehemu mbalimbali za mji huo, vikiwemo kiwanda cha chuma, kiwanda cha simenti, na kiwanda cha kutengenezea mawe ya lami, huku vikiwa karibu na nyumba za watu.
Bwana Kieti, pamoja na mke wake na watoto, wanaishi karibu na kiwanda cha lami ambacho kinatoa harufu mbaya na hewa nzito ya moshi, na kupelekea kulifunika eneo hilo na moshi mweusi.
Shirika la afya dunia linasema kiwango cha hewa chafu kimefikia asilimia 70 juu ya kiwango kinachoruhusiwa mjini Nairobi.
Ni mchanganyiko unaosababishwa moshi mzito kutoka kwenye magari ya zamani, takataka zinazochomwa moto na viwanda.
'Code for Africa' huleta mashine hizi ili kusaidia wanaharakati wenye hofu juu ya uchafuzi wa hewa.
Msemaji wa Code for Africa, Yazmin Jumaali amesema ''Takwimu zetu ni za uhalisia, kwa hiyo mtu yoyote anaweza kuzitumia.
Wanaweza kupata takwimu za kila siku ambazo wanaweza kutumia kwenye kampeni za kuitaka serikali kutatua matatizo wanayokabiliana nayo kuhusu uchafuzi wa hewa''
''Majibu yalikuwa ni ya kushangaza sana. Mashine ilikuwa inaonyesha kuwa hewa ilikuwa chafu kwa kiwango kikubwa sana.'' Alisema Bwana Kieti.
Mashine hizi zilionyesha chembechembe za hewa hatari zenye kiwango cha (PM2.5), ambazo ni za mikromita 2.5 na ndogo zaidi katika kipenyo, kama udogo wa mara 20 hivi ukilinganisha na mchanga, vili vile udogo wake unaamnisha vinaweza kuingia kwenye damu.
Takwimu hizi zimechapishwa katika tovuti, ambapo mtu yoyote anaweza kuzipata kwa bure.
''Tulikuwa tukiamka usiku kuangalia thamani ya hewa na kuzipiga picha ili tuweze kuzitumia katika kampeni zetu.'' Amesema Bwana Kieti.
Mwezi Juni Bwana Kieti na wenzake kutoka katika jamii hiyo walianzisha kampeni katika mitandao ya kijamii wakiwaonesha wengine takwimu walizozipata.
''Tulitumia mitandao ya Twitter, Facebook, Whatsapp, na Youtube kuanzisha kampeni hizi kuonesha matokeo kutoka kwenye mashine kama njia ya kudai hewa safi.''
''Tulifanya mamlaka ya Taifa inayosimamia Mazingira wakose raha kwa kuwahusisha wengine(tag) katika ujumbe wa kwenye mitandao.
Vyombo vya habari vikaanza kutangaza kampeni hii, wakiangazia mambo mengi kuhusu uchafuzi wa hewa.
Sio tu kwa eneo la Bwana Kieti, lakini kila sehemu katika mjii mkuu wa Kenya.
Katika umbali wa dakika 30 kutoka Syokimau, kuna familia ambayo wanahofia kuwa mtoto wao ni muathirika wa hewa chafu.
Rashidah na Nazir Hakada wanaishi katika jimbo la Sawada, ambalo nalo lina viwanda kadhaa.
Bado wanaomboleza kifo cha mtoto wao Hafsa, aliyekuwa na umri wa miaka miwili, ambaye alifariki dunia mwezi Juni baada ya kupatwa na maambukizi katika njia ya hewa na kusababisha mapafu kudhoofika na kushindwa kutengeneza oksijeni ya kutosha kwendakwa viungo muhimu mwilini.
Madaktari wanasema tatizo hilo linaweza sababishwa na viwango vya juu vya moshi au moshi wa kemikali.
''Mtoto wetu alikuwa na matatizo ya kupumua. Mara ya kwanza alilazwa mwezi Aprili, wakaturuhusu tukarudi nyumbani.
Akalazwa tena mwezi Juni kwa tatizo hilo hilo, akakaa hospitalini kwa saa 48 baada ya hapo alifariki dunia.'' Amesema bwana Hakada.
Wanandoa hao wana watoto wawili wengine, na mmoja wao alilazwa hivi karibuni kwa sababu ya matatizo ya kupumua.
''Angalia mashine hizi zote za kumsaidia kupumua,'' Bi. Hakaada akisema kwa hasira akichambua mashine za kuwasaidia watu wenye ugonjwa wa pumu.
''Ni uonevu kwake. Ana miaka 6 tu.''
''Akikohoa, basi anakohoa wiki nzima. Ni mtoto mdogo sana na dhaifu.''
Bwana Hakada na wenzake katika jamii yao wameweka mashine katika jimbo lao. Na kama vile Syokimau, wanatumia takwimu zao kudai hewa safi.
Vikwazo havipo tena'
Wamependa kazi za Bwana Kieti na vile juhusu zake zilivyo zaa matunda.
'' Hatimaye maafisa wa mazingira wamesikia kilio chetu baada ya kutokututilia maanani kwa muda mrefu.'' Ameeleza.
''Walikuja na kukagua kiwanda, na kuzungumza na watu wa jamii yetu na kuitaka kiwanda hicho kifungwe hadi pale watakapoleta mashine ya kuchujia hewa.''
Na sasa, mashine zinarekodi kiwango kidogo cha hewa chafu.
''Tumefurahi sana kuona kampeni yetu imezaa matunda. Moshi mzito na mkali haupo tena.''
Kiwango ambacho watoto wetu walikuwa wakiumwa maambukizi ya vifua inapungua.
Aliyasema akiwa anatabasamu huku akizungumzia mafanikio yao.