Shirika la afya duniani: Ukosefu wa mazoezi kwa watoto huathiri afya zao

Children watching TV

Chanzo cha picha, Science Photo Library

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa, watoto wanne kati ya watano wenye umri wa miaka 11-17 duniani hawafanyi mazoezi ya viungo ya kutosha.

Shirika la afya duniani (WHO) limesema kuwa afya za watoto zinaharibiwa kutokana na ukosefu wa mazoezi hivyo kuathiri ukuaji wa ubongo na shughuli zao za ujuzi kupungua uwezo.

Utafiti huo umesema kwamba chanzo ni kutokufanya mazoezi, inashauriwa kuwa ni vyema mtoto kufanya mazoezi walau kwa saa moja kwa siku.

Tatizo hili limekuwa kubwa duniani kote katika mataifa maskini na tajiri.

Watoto wa kiume wanaoneka kujishughulisha zaidi katika kufanya mazoezi kuliko watoto wa kike katika nchi 4 kati ya 146 zilizofanyiwa utafiti.

Mazoezi gani wanapaswa kuyafanya?

Mazoezi yoyote yanayofanya mapigo ya moyo yaende kwa haraka na mapafu kupumua kwa nguvu, kama vile;

-Kukimbia

-Kuendesha baiskeli

-Kuogelea

-Kucheza mpira

-Kuruka kwa mguu mmoja

-Kuruka Kamba

-Sarakasi

Daktari kutoka shirika la afya dunia, Dkt Fiona Bull amesema kuwa hadhani kwamba ni lengo kubwa sana la kujiwekea lakini ni vyema kuzingatia afya.

''Ni vizuri kujijengea afya nzuri na maendeleo ya mwili.''

Skateboarder

Chanzo cha picha, Getty Images

Tofauti kati ya mazoezi ya wastani na yale ya kutumia nguvu ni kwamba mazoezi ya wastani unakuwa unaweza kuzungumza lakini ya mazoezi ya nguvu hayakuruhusu kuzungumza, kwa sababu unakuwa hauna pumzi ya kutosha.

Kwanini ni muhimu kujali?

Sababu kubwa ni afya ya sasa hivi na ya baadae.

Kwa muda huu mfupi, kuwa mchamgamfu kunamaanisha:

-Moyo na mapafu yanakuwa na afya

-Mifupa na misuli imara

-Afya ya akili ya mwili inakuwa nzuri

-Uzito mdogo

Pupil working

Chanzo cha picha, Getty Images

''Vijana wachangamfu wana uwezekano wa kuwa watu wazima wachangamfu,'' Anaeleza Daktari kutoka shirika la afya duniani.

Na vilevile muda unavyozidi kwenda basi unapunguza hatari ya kupata magonjwa kama mshtuko wa moyo, kiharusi, na aina ya pili ya ugonjwa wa kisukari.

Girls playing volleyball

Chanzo cha picha, Getty Images

Ukosefu wa mazoezi unamuweka mtu mmoja kati ya watu wazima wanne hatarini.

Lakini uchunguzi unasema kuwa kuna ushahidi wa kutosha unaoonesha kujishughulisha ni kitu kizuri kwa ukuaji wa ubongo.

''Wanakuwa na uwezo wa kutambua, kujifunza kwa urahisi, na tabia nzuri ya kujichanganya na wengi.'' Amesema Dkt Guthold.

Je kwa kawaida watoto ni wavivu tu?

Je, utafiti huu unatuambia nini kuhusu misingi ya watoto?

Dkt Bull amesema kuwa ''Watoto sio wavivu''

''Hii inatueleza kuhusu kitu kikubwa zaidi lakini sio kuhusu watoto peke yake.