Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Rais Museveni ammwagia sifa Donald Trump
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema anampenda rais wa Marekani Donald Trump katika hotuba yake wakati wa ufunguzi wa bunge la Afrika Mashariki jijini Kampala.
Museveni alisema Marekani ina rais mzuri sana wakati wa ufunguzi wa mkutano huo wa bunge la Afrka mashariki.
''Ninampenda trump kwasababu anasema ukweli mtupu, waafrika wanatakiwa kusuhisha matatizo yao wenyewe, Waafrika ni dhaifu sana'' Museveni.
Pongezi hizo za museven kwa Trump zinakuja saa chache tuu baada ya balozi wa Uganda kwa Marekani Deborah Malac kumkosoa Trump.
''Kauli zake zinachukiza na kukera sana'' amesema Deborah.
Maoni hayo ya rais Museveni ni tofauti sana na viongozi wengi wanaochukizwa na kauli za Trump.
Mapema mwezi huu Trump alidaiwa kutoa kauli za kejeli juu ya nchi za Afrika wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya wahamiaji.
Trump alikataa kuwa ametoa kauli hizo za kejeli lakini seneta mmoja aliyehudhuria mkutano huo alisema kuwa Trump alitamka maneno ya kejeli na matusi kwa nchi kama Haiti, elsalvador na nchi za Afrika.
Kwa mujibu wa gazeti la New York times, mwaka jana Trump alisema kuwa watu wote wanaotoka Haiti wana ukimwi, na wananigeria wakiruhusiwa kuingia marekani basi watakataa kurudi Kwao.
Ikulu ya White House ilikanusha madai ya kauli hizo.