Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Maandamano dhidi ya rais Macky Sall yafanyika Senegal
Maelfu ya watu wamefanya maandamano leo katika mji mkuu wa Senegal, Dakar, kupinga uongozi wa Rais Macky Sall.
Wanataka kuachiliwa kwa wapinzani wa kisiasa wa Rais hasa, Meya wa Dakar, Khalifa Sall.
Amekuwa kuzuizini kwa mwezi mmoja kwa madai kuwa alishiriki katika kulaghai serikali kiasi kikubwa cha pesa.
Anaonekana na wengi kama mshindani mkali katika uchaguzi wa Urais utakaofanywa mwaka 2019 akiwa mshindani wa chama cha Socialist Party.
Maandamano hayo yaliandaliwa na kundi linalojiita "tumechoka" lililoundwa miaka mitano iliyopita dhidi ya aliyekuwa Rais wa zamani, Abdoulaye Wade.