Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Marekani yakatiza ufadhili kwa UNFPA linalohusika na mpango wa uzazi
Marekani imesitisha ufadhili kwa mfuko wa Umoja wa Mataifa wa idadi ya watu, UNFPA unaotoa msaada kwa ajili ya mpango wa uzazi kote duniani.
Hatua hiyo italifanya shirika hilo la Umoja wa Mataifa kupoteza takriban dola milioni thelathini za ufadhili kwa mwaka huu pekee.
UNFPA limepinga madai kuwa linafadhilili shughuli za uaviaji mimba.
Hili ni shirika la kwanza la Umoja wa mataifa kukabiliwa na kupunguwa kwa ufadhili baada ya ahadi ya kupunguza msaada wa kifedha kutoka kwa utawala wa Trump.
Hii ina maana kuwa UNFPA litapoteza ufadhili wa siku zijazo zikiwemo dola milioni 32.5 zilizokuwa zimepangwa kutumiwa mwaka huu.
Wizara ya mambo ya nje Marekani inasema kuwa uamuzi huo ulizingatia shughuli za UNFPA za mpango wake wa uzazi na serikali ya Uchina, ambazo inasema ulisaidia kuavya mimba na kufunga uzazi kwa lzima.
Badala yake ufadhili huo utaelekezwa katika mipango mingine ya uzazi katika nchi zinazoendelea.
Shirika hilo hatahivyo limesema kuwa madai hayo ''si sahihi'', na kwamba kazi zake zote zimekuwa ni za kuboresha haki za kibinfasi na wanandoa kuchukua maamuzi yao bila ubaguzi.