Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ufaransa na katazo la vazi la Burkini,katika pwani zake
Mahakama moja nchini Ufaransa iliyoko pwani ya mji wa Corsica, imesita kutoa amri ya katazo kwa wanawake wavaa vazi la burkini,vazi hilo ambalo mwanamke avaapo huanzia kichwani na kustiri mwili wote, na hupendwa mno na wanawake wa Kiislam.
Mwezi uliopita, mahakama ya juu nchini Ufaransa ilitoa uamuzi wa kupiga marufuku uvaaji wa burkini katika pwani zake kuwa ni kinyume na katiba na ukiukwaji uhuru wa umma .
Kufuatia katazo hilo Meya mmoja alitoa mari ya kusitisha na kupekuliwa kwa wanawake watakaokuwa wamevaa burkini baada ya mvutano wa waliokuwa wamevaa vazi hilo pwani wakati wa mapumziko .