Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mourinho: Wenger na Klopp hawana ''maadili''
Mkufunzi wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho anasema kuwa ukosoaji uliotolewa na kocha wa Arsenal Arsene Wenger na mwenzake wa Liverpool Jurgen Klopp ''hauna maadili''.
Wenger na Klopp wamelalamikia uhamisho wa pauni milioni 100 wa Paul Pogba.
''Kuna vitu ambavyo nikifanya havina maadili,lakini wengine wakifanya ni jambo la kawaida'',alisema Mourinho.
Mkufunzi huyo wa United ameongezea kuwa atamsajili mchezaji mzuri wa kiungo cha kati katika siku chache zijazo na Pogba ni muhimu.
''Kwa sasa tuna wachezaji 22,alisema.Tutakuwa na 23.Ni mchezaji wa Juve hadi pale atakapokuwa rasmi nje''.Soko la uhamisho linafungwa tarehe 31 mwezi Agosti.
''Tunajaribu kila tuwezalo kufunga soko letu la ununuzi kwa haraka iwezekanavyo''.