Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Salah kuiongoza Misri dhidi ya Senegal ya Mane fainali ya Afcon baada ya kuilaza Cameroon
Kipa Gabaski ndiye aliyekuwa shujaa , baada ya kuokoa mikwaju miwili ya penalti na kuisaidia Misri kuwaondoa katika michuano hiyo wenyeji Cameroon katika mechi ilioamuliwa na mikwaju ya penalti kufuatia sare ya bila kwa bila .
Hatua hiyo sasa itazikutanisha Misri na Senegel katika fainali ya Afcon siku ya Jumapili.
Fainali hiyo itawakutanisha washambuliaji wawili wa Liverpool Mohammed Salah dhidi ya Sadio Mane katika uwanja huohuo - wa Olembe uliopo katika mji mkuu wa Younde
Wenyeji Cameroon walionesha mchezo mzuri na ari katika dakika tisa za mechi hiyo , mara mbili wakigonga chuma cha goli kupitia kichwa cha mchezaji Ngadeu -Ngadjui na shambulizi kali la Samuel Gouet ambalo pia lilipanguliwa na chuma cha goli.
Nyota wa Misri Mo Salah alinyamazishwa katika kipidi kirefu cha mechi , akifanikiwa kupinda shambulio moja ambalo halikulenga goli la upinzani .
lakini hakupiga penalti baada ya wachezaji wa Cameroon kushindwa mara tatu kucheka na wavu , huku Gabaski akiokoa kutoka kwa mkwaju wa Harold Moukoudi na James Siliki naye Clinton N'jie akipiga nje.
Mechi hiyo iliojawa na ghadhabu katika dakika za lala salama ilimfanya mkufunzi wa Misri Carlos Quiroz kupigwa kadi nyekundu kwa kupinga maamuzi ya refa na wasaidizi wake kwa hasira huku Wael Gomaa naye pia akionywa.
Hii ina maana kwamba makocha wote wawili hawatakuwepo katika fainali baada ya Goma kupi gwa kadi ya njano katika mechi ya robo fainali dhidi ya Morocco
Wakati huohuo, Cameroon itachuana na Burkina Faso ili kupata mshindi wa tatu mechi itakayochezwa siku ya Jumamosi.
Misri yalipiza kisasai dhidi ya Cameroon
Huu ulikuwa mkutano kati ya timu mbili zilizofanikiwa zaidi katika historia ya mashindano hayo huku Misri ikifanikiwa kushinda mara saba dhidi ya Cameroon.
Wenyeji walifanikiwa kushinda mara tano huku mara ya mwisho ikiwa 2017, wakati walipowashinda wapinzani wa Ahamisi 2-2 katika fainali , lakini Misri imelipiza kisasi sasa.
Mbali na mechi hiyo kuwakutanisha washambuliaji wa Liverpool Salah na Mane , fainali hiyo itakuwa ya kwanza katika ya mechi tatu kati ya Misri na Senegal katika kipindi cha miezi miwili , kwa kuwa watalazimika kuamua mshindi atakayewakilisha Afrika katika kombe la dunian nchini Qatar.
Kulikuwa na maandalizi makali kabla ya mechi hiyo huku rais wa shirikisho la soka nchini Cameroon Samuel Etoo akiitaja mechi hiyo kuwa 'vita' katika hotuba yake.
Lakini mkufunzi wa Misri Queiroz alihisi ilikuwa picha mbaya hususan baada ya watu wanane kufariki na wengine 38 kujeruhiwa katika mkanyagano katika uwanja huo wa Olembe.
Macho yote yalikuwa yameelekezwa kwa Salah, ambaye shambulio lake la kuupinda mpira baada ya dakika nane halikufaulu, lakini Cameroon ilitawala kipindi kirefu cha mchezo huku kichwa cha Ngadeu Ngadjui kikipiga chuma cha goli na beki huyo akakosa bao la wazi akiwa maguu sita katika lango la upinzani na kusababisha mpira wa kupigwa kona.
Salah alijaribu kufunga katika kipindi cha pili lakini kipa wa Cameroon Andre Onana alikuwa macho .
Kichwa cha Karl Toko Ekambi baadaye kilinyakwa na kipa Debask, huku shambulio zito la Gouet lililochukuliwa na kipa Debask karibia liiweke kifua mbele Cameroon huku mechi ikienda katika muda wa ziada.
Free kick iliopigwa na kiungo wa kati wa Middlesborough Lea Siliki ilipaa katika dari ya neti, na kufanya mchuano huo kufika katika mikwaju ya penalti.
Gebask ambaye aliingia baada ya kipa wa kikosi cha kwanza cha Misri Mohammed Shenawy kupata jeraha katika mechi ya mwisho ya ushindi dhidi ya Ivory Coast , alisaidia timu yake na kuhakikisha kuwa imeshinda mara sita katika upigaji wa penalti ili kusonga mbele.