Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Afcon 2021: Senegal yailaza Burkina Faso 3-1 na kutinga fainali Afcon
Senegal imefuzu katika fainali yao ya tatu ya kombe la bara Africa huku Sadio Mane akifunga na kuwasaidia kuwalaza Burkina Faso .
Katika mechi iliojaa mbwembwe na bashasha , VAR ilifuta malalamishi mawili ya Senegal ya penalti , huku kipa wa Burkina Faso Herve Koffi akijeruhiwa katika tukio la kwanza .
Abdou Diallo na Idrissa Gueye waliipatia uongozi Senegal kabla ya Blati Toure kupunguza uongozi huo wakati wa muda wa lala salama.
Lakini Mane alifunga goli la tatu na kuipatia timu yake ushindi mkubwa. Lilikuwa goli la 29 la Mane kwa taifa lake , na kumuweka sawa na aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo Henry Camara.
Senegal sasa itakabiliana na Misri au waandaji wa dimba hilo Cameroon katika fainali ya siku ya Jumapili.
Burkina Faso nayo itashiriki katika mechi ya kutafuta mshindi wa tatu wa mashindano hayo ambayo itachezwa siku moja kabla ya fainali hiyo.
"Inaonesha ari yetu'' , alisema Mane . Tulijua haitakuwa rahisi kufuzu katika fainali ya pili mfululizo , lakini kitu muhimu kwetu sisi sasa ni kwenda na kushinda bila kujali timu tutakayokutana nayo fainali''. Tulikabiliana dhidi ya kikosi kizuri sana cha Burkina Faso ambacho kilikuwa hatari sana''.
''Tulitaraji mechi ngumu na kama ilivyokuwa , lakini tulicheza mchezo makini na kubuni fursa chungu nzima , nadhani ilikuwa haki yetu kupata ushindi''.
''Nadhani unaweza kuona sura yangu ilivyojaa na furaha , ambacho ni kitu cha kawaida. Kwa kweli najivunia mimi binafsi , wachezaji wenzangu na taifa langu''.
Senegal imeshiriki katika fainali mbili za michuano hiyo bila kuandikisha ushindi wowote 2002 na 2019.
Dakika nne tu baada ya kipute hicho kuanza, katika uwanja wa Ahmadou Ahidjo Stadium katika mji mkuu wa Cameroon Yaounde, wachezaji wawili Nampalys Mendy na Cyrille Bayala waligongana vichwa wakigombania mpira.
Hali hiyo ilizua kinyang'anyiro kilichosheheni makabiliano makali kati ya timu mbili ambazo zimefika fainali ya michuano hiyo awali lakini hazijawahi kupata ushindi.
Senegal ndio taifa lililoorodheshwa bora zaidi katika orodha ya Fifa Africa likiwa katika nambari ya 20 duniani, na umahiri wao ulionekana.
Walipata nafasi za kwanza za kujiweka kifua mbele , huku Kofi akigongana na Cheikhou Kouyate naye Edmond Tapsoba akimpiga kisukusu Idrissa Gueye katika kabiliano lililoonekana kuwa penalti.
Lakini nafasi hizo zote zilikataliwa na refa Bamlka Tessema Weyesa baada ya kutakiwa kuangalia katika runinga ya VAR.
Burkina faso waligharamika , huku Koffi akilazima kutolewa nje katika dakika ya 36 baada ya kumuangukia vibaya kiungo wa kati wa Crystal Palace Kouyate akijaribu kuupangua mpira.