Afcon 2021: Mabingwa watetezi waondolewa na Ivory Coast baada ya kushindwa 3-1

Mabingwa watetezi Algeria wametemwa katika kombe la mataifa ya Afrika kufuatia kichapo cha mabao 3 -1 dhidi ya Ivory Coast huko Douala.

Algeria ilijikokota kwa tofauti ya magoli mawili katika kipindi cha mapumziko baada ya Ibrahim Sangare kupokea pasi safi kutoka kwa Franke Kessie na kulipachika goli wavuni.

Nicolas Pepe anayeichezea Arsenal aliipatia Ivory Coast uongozi wa 3-0 kabla ya nahodha wa Algeria Riyad Mahrez kupoteza penalty kwa kugonga chuma.

Sofiane Bendebka aliifungia Algeria bao la kufutia machozi dakika za mwisho na kuifanya sasa timu hiyo kuyaaga mashindano hayo ikiwa katika Kundi E chini baada ya ushindani mkali.

Kikosi cha Djamel Belmadi ni mabingwa wa tatu watetezi kuondoka katika awamu ya kwanza ya mashindano katika fainali tano zilizopita za kuwania kombe hilo la mataifa ya Afrika.

Kuondokwa kwao kutoka mashindano hayo ni tofauti na timu hiyo ilivyoingia, ikielekea Cameroon ikiwa ina ushindi wa kutopingwa wa mechi 34 na ilitarajia kuipiku rekodi ya Italia ya ushindi mfululizo wa mechi 37.

Algeria ilitoka sare ya 0-0 dhidi ya Sierra Leone kabla ya kushindwa 1-0 dhidi ya Guinea ya Ikweta na inaondoka na pointi moja kutoka mechi tatu - lakini angalau ilifanikiwa kufunga bao kupitia mkwaju wa dakika za mwisho wa Bendebka - uliotoa matumaini ya ushindani.

Tembo wa Ivory Coast waliongoza kundi lao na kujinyakulia fursa ya kukutana na Misri katika mechi ya timu 16 za mwisho inayotarajiwa kupigwa Jumatano Januari 26.

Gumzo kubwa lilikuwa kuhusu hali duni ya uwanja wa Japoma kabla ya mechi hiyo wakati mabingwa wawili wa hivi karibuni - Ivory Coast ikiwa mshindi mnamo 2015 - walipokutana katika mchuano wa mwisho wa makundi, uliokuwa kama sherehe kuu.

Kocha wa Algeria Belmadi alishangazwa na ukame wa magoli wa timu yake na wakati Ismael Bennacer alipolinusa lango la upinzani kunako dakika 22, ila Ivory Coast ililipiza kwa bao dakika moja tu baadaye, huenda alihisi hali ni mbaya.

Pasi muruwa kutoka kwa Max-Alain Gradel iliutingisa wavu wavu na kupelekea nderemo kubwa wakati wachezaji wa ziada 12 wa Ivvory Coast walipomiminika kusherehekea na nyota huyo wa timu ya AC Milan na kuiwacha Algeria ikihitaji magoli mawili ili kupata ushindi .

Wachezaji hao wa Afrika kaskazini walipigwa na butwaa na hali ilizidi kudorora wakati Tembo walipotumia shinikizo kuongeza bao la pili wakati Sangare alipoachwa peke yake kulisukuma tobwe nyumbani baada ya kupokea krosi muruwa kutoka kwake Serge Aurier.

Belmadi alifahamu fikra kwamba muongozo atakaokipatia kikosi wakati wa muda wa mapumziko ulikuwa muhimu sana lakin badala yake miamba hiyo ya soka kutoka Afrika magharibi waliendeleza kampeni na kupata fursa mara mbili kabla ya Pepe kufunga goli la kishindo.

Hapakuwa na shaka kwamba ushindani ulikuwa sio wa Algeria na zaidi baada ya Mahrez wa Algeria aliyehamia Manchester City hivi karibuni kukosa penalti kunako dakika 60 na kuishia kugonga chuma baada ya Youcef Belaili kuangushwa.

Tembo wanaojiamini

Wakati umma wa mashabiki ulianza kuonyesha kwa kelele kuridhishwa, kocha wa Ivory Coast Patrice Beaumelle alianza kuwapumzisha wachezaji kwa kufanya mabadiliko kabla ya Bendebka kuirudishia heshima timu ambayo ililinyayua taji mjini Cairo miaka mitatu iliyopita.

Mshambuliaji wa Ajax Sebastien Haller alidhani amesukuma tobwe la nne, na la pili katika mashindano hayo, aliposukuma krosi aliopokea kutoka Aurier lakini lilikataliwa na kusemekana lilikuwa ni la kuotea.

Kwa kujiamini, na nguvu na ari timu ya Ivory Coast ilistahili ushindi uliowaacha wachezaji wa Algeria sakafuni, wakizubaa kwa mshangao kuhusu namna walivyotolewa katika mashindano hayo.

Imekuwa timu ya 12 ya bingwa mtetezi kutolewa katika mashindano hayo katika awamu ya kwanza wakitetea taji.

Mashabiki waliuvamia uwanja na kufika karibu ya wachezaji wakati kipenga cha mwisho kilipopulizwa, kabla ya maafisa wa usalama kuingia kwa kuchelewa kujaribu kutuliza hali.

Tayari Douala inachunguzwa kwa kiwango cha uwanja - kuchangia mapendekezo ya kuhamishwa mechi kutoka mji huo mkubwa wa Cameroon.