Messi, Ronaldo na Salah katika orodha ya wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa FIFA

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Mshambulizi wa Paris St Germain Lionel Messi, Cristiano Ronaldo wa Manchester United na Mohamed Salah wa Liverpool ni miongoni mwa wachezaji 11 walioteuliwa kuwania tuzo ya Mchezaji Bora wa FIFA kwa Wanaume, shirikisho la soka duniani lilisema Jumatatu.

Watatu hao wameungana na mshindi wa mwaka jana Robert Lewandowski wa Bayern Munich, mchezaji wa Manchester City Kevin De Bruyne na wachezaji wawili wa Chelsea N'Golo Kante na Jorginho.

Mshambulizi wa Real Madrid Karim Benzema, mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Haaland na nyota wa PSG Kylian Mbappe na Neymar wanakamilisha orodha hiyo.

Wachezaji wa Super League ya Wanawake wanatawala tuzo ya wanawake huku Vivianne Miedema wa Arsenal, Wachezaji wawili wa City Lucy Bronze na Ellen White na wachezaji wanne wa Chelsea Sam Kerr, Magdalena Eriksson, Pernille Harder na Ji So-yun wakiwania.

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Emma Hayes, ambaye aliiongoza Chelsea kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa 2021, amejumuishwa kwenye orodha ya mchujo ya Kocha Bora wa FIFA kwa Wanawake na meneja wa Uingereza Sarina Wiegman na kocha wa Canada Beverly Priestman.

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola, Thomas Tuchel wa Chelsea na mkufunzi wa Tottenham Hotspur Antonio Conte wameteuliwa kuwania tuzo ya wanaume, pamoja na Mjerumani Hansi Flick na kocha wa Italia Roberto Mancini, ambaye aliwaongoza kutwaa ubingwa wa Euro 2020.

Alisson Becker wa Liverpool, Edouard Mendy wa Chelsea na Kasper Schmeichel wa Leicester City ni miongoni mwa walioteuliwa kuwania tuzo ya Kipa Bora wa FIFA kwa Wanaume.

Washindi watatangazwa Januari 17.