Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 22.11.2021: Pochettino, Ten Hag, Mount, Messi, Barisic

Mauricio Pochettino

Chanzo cha picha, Reuters

Mauricio Pochettino yuko tayari kuwa meneja wa Manchester United na hakuna shaka kwamba wanaweza kumpata kocha wa Paris St-Germain sasa.

Muargentina huyo anaheshimika sana Old Trafford lakini kulikuwa na hisia kuwa inaweza kuwa vigumu kumshawishi kutoka PSG katikati ya msimu.

United ilimtimua Ole Gunnar Solskjaer siku ya Jumapili na kusema walikuwa wanatafuta kumteua meneja wa muda.

Lakini uwezekano wa kupatikana kwa Pochettino unaweza kubadilisha hilo.

Ten Hag alijibu uvumi kwamba atachukua mahala pake Ole Gunnar Solskjaer katika klabu ya Man United kwa kusema kwamba hajasikia ombi lolote kutoka kwa klabu hiyo. (Manchester Evening News)

Lopetagui

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Lopetagui

Wakala wa Kireno Jorge Mendes anaisukuma Man United kujaza pengo la Ole Gunnar Solksjaer kwa kumuajiri mkufunzi wa Sevilla Julen Lopetegui. Raia huyo wa Uhispania ana kandarasi na klabu hiyo hadi 2024 lakini Mendes ambaye anamuwakilisha Cristiano Ronaldo anamtaka kuchukua kazi hiyo Old Trafford. (Manchester Evening News)

Mkufunzi wa Uhispania Luis Enrique amekana madai yanayomuhusisha na klabu ya Manchester United. (Goal)

Real Madrid ina hamu ya kumsajili kiungo wa Chelsea na England Mason Mount. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 yupo katika mazungumzo na klabu hiyo kuhusu mkataba mpya , ijapokuwa inasemekana anahisi hapendwi na huenda akajiandaa kuondoka. Klabu za Manchester City na Bayern pia zina hamu naye.. (Fichajes - in Spanish)

Mason Mount

Chanzo cha picha, Getty Images

Mkufunzi mpya wa klabu ya Aston Villa Steven Gerrard anataka kumsaini beki wa kushoto wa Croatia Borna Barisic, 29, kutoka klabu yake ya zamani Rangers. (Daily Record)

Mkufunzi wa Everton Rafael Benitez anasema kwamba klabu hiyo itahitaji kuwasaini wachezaji wapya katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari huku winga wa England Demarai Gray, 25, akiwa mchezaji wa hivi karibuni kupata jeraha wakati wa mechi waliopoteza kwa Mchester City.. (Liverpool Echo)

Messi

Mshambuliaji wa PSG Lionel Messi, 34, hana mpango wa kurudi Barcelona baada ya rais wa klabu hiyo Joan laporta kusema kwamba klabu hiyo ya Uhispania inaweza kumsajili raia huyo wa Argentina katika siku za usoni.. (AS)

Mkufunzi mpya wa Barcelona Xavi ana hamu ya kumsaini mshambuliaji wa Algeria Baghdad Bounedjah ,29 kutoka klabu ya zamani ya Al-Sadd nchini Qatar. (Sport - in Spanish)