Rais wa Rwanda Paul Kagame amefadhaishwa na kushindwa kwa Arsenal

Muda wa kusoma: Dakika 1

Rais wa Rwanda na shabiiki wa Arsenal Paul Kagame ameelezea kughabishwa kwake na hatua ya Gunners kushindwa na klabu ya mpya iliyopandishwa daraja katika mechi ya ufunguzi ya Ligi kuu ya Uingereza.

Brentford, iliyorejea katika ligi hiyo baada ya miaka 74 iliishabanga Arsenal mabao 2-1.

Bw Kagame mara kwa mara huangazia Gunners - klabu ambayo serikali yake ilifadhili.

Baada ya mechi hiyo aliandika katika mtandao wake wa Twitter: "Hatupaswi tu kutoa udhuru au Kukubali upuzi. Timu lazima iiundwe kwa lengo la kushinda kushinda na kushinda."

Katika ujumbe mwingine alitaka wawe na "mpango utakaozaa matunda" ma kulalamika kwamba "mashabiki hawahitaji kuzoea hali hii".

Tanngu mwaka 2018, serikali ya Rwanda imekuwa na makubaliano ya udhamini yenye utata ya thamani ya zaidi ya pauni milioni 30 ($ 42m), ambayo inajumuisha nembo ya "Tembelea Rwanda" inaoonyeshwa kwenye mikono ya fulana ya Arsenal.

Wakosoaji wamesema ni mfano wa kiongozi wa kimabavu wa nchi masikini, ya Kiafrika inayofadhili kilabu tajiri cha mpira. Lakini serikali ya Rwanda inasema udhamini huo zaidi ya unajilipa kupitia mapato ya utalii..

Matokeo ya mechi Jumamosi

Katika mechi za EPL zilizochezwa leo Jumamosi;

Manchester United 5-1 Leeds United

Burnley 1- 2 Brighton

Chelsea3 - 0 Crystal Palace

Everton3- 1 Southampton

Leicester 1-0 Wolves

Watford 3-2 Aston Villa