Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 14.08.2021: Mbappe, Milenkovic, Odegaard, Aubameyang, Kane, Torres

Mshambuliaji wa Paris Saint-Germain Kylian Mbappe

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mbappe alikuwa katika kikosi cha Ufaransa kilichoshinda Kombe la Dunia mwaka 2018

Real Madrid wanajiandaa kuwasilisha dau la euro milioni 120 (£102m) kumsajili mshambuliaji wa miaka 22 wa Ufaransa Kylian Mbappe kutoka Paris St-Germain msimu huu wa joto. (Cadena SER - in Spanish)

Tottenham wako tayari kumnunua beki wa Villarreal na Uhispania Pau Torres, 24, ambaye bei yake inakadiriwa kuwa pauni milioni 55. Torres pia ananyatiwa Manchester City, Liverpool na Manchester United. (Times - subscription required)

Spurs pia wamefanya mazungumzo na Fiorentina kuhusu mkataba wa mlinzi wa Serbia mwenye umri wa miaka 23 Nikola Milenkovic, ambaye pendekezo lake la kuhamia West Ham liligonga mwamba. (Sky Sports)

Pierre-Emerick Aubameyang

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Arsenal iko tayari kumuuza mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang

Arsenal wako tayari kupokea ofa ya kumuuza mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang,32. ( Times, usajili unahitajika)

Mshambuliaji wa Tottenham na Harry Kane, 28, atakutana na Manchester City wanaotaka kumnunua kwa pauni milioni 150 Jumapili hii. (Mail)

City huenda wakawasilisha dau lingine kumpata Kane kutika mkutano wa wikendi hii na Spurs. (MEN)

Liverpool bado wanataka kumsaini winga wa Wolves na Uhispania Adama Traore, 25, kabla dirisha la uhamisho kufungwa. (90min)

Adama Traore

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Liverpool bado wanamtaka winga wa Wolves na Uhispania Adama Traore

Real Madrid wanajiandaa kumuuza kiungo wa kati wa Norway Martin Odegaard msimu huu wa joto. Arsenal wako tayari kuwasilisha dau la kumnunua kiungo huyo wa miaka 22- ambaye alipata ufanisi mkubwa katika mkataba wake wa bure na Gunners msimu ulliopita. (Goal)

Odegaard hatajumuishwa katika kikosi cha Real Madrid wakati wa mechi ya ufunguzi wa La Liga, lakini huenda akagharimu kati ya pauni milioni 35-40. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Lautaro Martinez, 23, ameamua kusalia katika klabu hiyo licha ya kunyatiwa na Tottenham na Arsenal. (Mirror)

Lautaro Martinez

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Lautaro Martinez, 23, ameamua kusalia Inter Milan Licha ya kunyatiwa na Tottenham na Arsenal

Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta huenda akamgeukia kipa wa Newcastle United Muingereza Freddie Woodman,24, baada ya kushindwa kumsaini kipa wa Sheffield United na England Aaron Ramsdale, 23. (Chronicle)

Mkufunzi wa Southampton Ralph Hasenhuttl hatarajii kiungo wa kati wa England James Ward-Prowse, 26, kuondoka klabu hiyo. Saints wamekataa dau la pauni milioni 25m kutoka kwa Aston Villa. (Daily Echo)

Tammy Abraham

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Roma yaimarisha juhudi za kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham

Meneja mkuu wa Roma Tiago Pinto ameweka "kadi zake zote mezani" ili kumshawishi mshambuliaji wa Chelsea na England Tammy Abraham,23, kujiunga na Serie A club. (Corriere dello Sport - in Italian)

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 21, ana 'ndoto' ya kuhamia Ligi ya Premia. (Sky Germany, via Star)