Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 29.04.2021: Sancho, Messi, Lukaku, Abraham, Demiral, Brandt, Kounde, Bellerin

Lukaku

Chanzo cha picha, Getty Images

Vigogo hao wa London maarufu kama the Blues wanaandaa kitita cha pauni milioni 90 ili kumrejesha klabuni hapo mshambuliaji wa klabu ya Inter Milan na timu ya taifa ya Ubelgiji, Romelu Lukaku, 27. (Sun)

Manchester United bado wanataka kufanya usajili wa winga wa kulia mwishoni mwa msimu, huku mchezaji nyota wa timu ya taifa ya England na klabu ya Borussia Dortmund Jadon Sancho, 21, akiendelea kuwa kipaumbele chao nambari moja. (90 Min)

Chelsea watapokea ofa za kuanzia pauni milioni 40 kwa klabu zitakazotaka kumsajili mshambuliaji wake Tammy Abraham, 23, mwishoni mwa msimu. (Telegraph - subscription required)

Jadon Sancho

Everton wanataka kumsajili beki wa Juventus na Uturuki Merih Demiral, 23. (Calciomercato - in Italian)

Arsenal wanajiandaa kumuuza beki wao wa pembeni Hector Bellerin, 26, na kuchukua nafasi yake wanataka kumsajili beki wa Norwich Max Aarons, 21. (90 min)

Beki wa kati wa Chelsea Fikayo Tomori, 23, amekutana na mkurugenzi wa klabu ya AC Milan Paolo Maldini. Milan wanataka kumsajili moja kwa moja mchezaji huyo ambaye sasa anaichezea klabu hiyo kwa mkopo. (Sky Sport - in Italian)

Fikayo Tomori kulia

Chanzo cha picha, Rex Features

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa Olivier Giroud, 34, hatarajiwi kuongeza mkataba na klabuyake ya Chelsea. (Goal)

Arsenal wanakusudia kumsajili kiungo wa Borussia Dortmund, Mjerumani Julian Brandt, 24. Usajili huo unaweza ukawa ni wa kuziba pengo la Martin Odegaard endapo kama Real Madrid watamtaka mchezaji wao huyo kurejea kikosini mwishoni mwa msimu. (Bild, via Mail)

Beki wa klabu ya Sevilla Jules Kounde, 22, ambaye alikuwa awali ananyemelewa na Chelsea sasa anawindwa na Real Madrid. (AS - in Spanish)

Burnley wapo tayari kutoa kitita cha pauni milioni 9 kumsajili beki Nathan Collins, 19, kutoka Stoke City. (Football Insider)