Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 12.04.2020: Kane, Martinez, Sancho, Upamecano, Kamara, Matic

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwenyekiti wa klabu ya Tottenham Daniel Levy anatarajiwa kuruhusu mshambuliaji wa klabu hiyo Harry Kane, 26, auzwe kwa klabu ya Manchester United kwa dau la pauni milioni 200 ili kutatua changamoto za kifedha za Spurs. (Mail)
Manchester City wanatarajiwa kuzipiku klabu za Chelsea, Real Madrid na Barcelona katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Lautaro Martinez, 22, mwenye thamani ya pauni milioni 97.5 . (Sun)
Klabu ya Newcastle inavutiwa na kumsajili kiungo wa Benfica na Ureno Rafa Silva, 26, lakini kwa sasa wamesimamisha mipango hiyo kutokana na mlipuko wa janga la virusi vya corona. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mbio za Liverpool kutaka kumsajili nyota wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya England Jadon Sancho, 20, zimegonga mwamba kutokana na dau lake na kuifanya Manchester United kubaki kuwa katika nafasi nzuri ya kumnyakua mshambuliaji huyo anayetajwa kwa na thamani ya pauni milioni 88. (Football Insider)
Klabu kadhaa za Ligi ya Primia zinazomnyemelea beki wa RB Leipzig Dayot Upamecano, 21 - zikiwemo Arsenal, Tottenham na Manchester City- zimekutana na kikwazo kutokana na klabu ya Real Madrid kutangaza kuwa tayari kumwania beki huyo wa kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa cha chini ya miaka 21. (Sunday Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester City wanajipanga kumsajili beki Boubacar Kamara, 20, kutoka klabu ya Marseille ambayo ipo tayari kumtoa beki huyo wa kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa cha chini ya miaka 21 kwa ada ya pauni milioni 28. (Express)
Kuimarika kwa kiwango cha kiungo mkabaji Nemanja Matic, 31, kumeilazimu klabu ya Manchester United kumpatia mkataba mpya. (Mail)

Chanzo cha picha, Matic
Shirikisho la Mpira Barani Ulaya (Uefa) linatarajia kukamilisha msimu huu wa michuano ya Klabu Bingwa Ulaya na Ligi ya Europa mwezi Agosti kwa kutumia kipindi cha wiki tatu. (Mirror)
Hasara inazopitia klabu za England zitaikumba klabu za bara lote la Ulaya endapo dirisha la usajili la majira ya kiangazi halitafanyika kutokana na virusi vya corona. (Sunday Telegraph)












