Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 27.01.2020: Bergwijn, Ben Yedder, Piatek, Rodriguez, Emre

James Rodriguez
Maelezo ya picha, Arsenal na Everton zinamnyatia James Rodriguez

Arsenal inatarajiwa kushindana na Everton katika kumsaini kiungo wa kati wa Real Madrid na Colombia James Rodriguez, 28. (AS, via Mail)

Tottenham inakaribia kumsaini mashambuliaji wa Uholanzi na klabu ya PSV Eindhoven Steven Bergwijn, 22. (Mirror)

Barcelona imetoa kitita cha £67m kumsaini mshambuliaji wa Monaco Wissam Ben Yedder. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa , 29, atajaza pengo lililowachwa na mshambuliaji Luis Suarez kupitia jeraha. (Foot Mercato)

Wissam Ben Yedder

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Barcelona imetoa kitita cha £67m kumsaini mshambuliaji wa Monaco Wissam Ben Yedder

Tottenham imeanzisha mazungumzo na AC Milan kuhusu mshambuliaji wa Poland Krzysztof Piatek, 24. (Sky Italia, via Mail)

Hatahivyo, Chelsea imedaiwa kupatiwa Piatek. (Star)

Uwezekano wa raia wa Saudia kuinunua Newcastle United itamfanya mmiliki mpya kumrudisha mkufunzi Rafael Benitez, ambaye ndie kocha wa klabu ya China ya Dalian Yifang. (Sun)

Manchester United imeongeza ombi lao la kutaka kumsaini kiungo wa kati wa Sporting Lisbon Bruno Fernandes kwa dau la awali la £46.4m lakini klabu hiyo ya Portugal inatarajia ofa bora zaidi kutoka kwa klabu nyengine ili kumuuza mchezaji huyo wa Portugal. (Times - subscription required)

Bruno Fernandes

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Manchester United imeongeza ombi lao la kutaka kumsaini kiungo wa kati wa Sporting Lisbon Bruno Fernandes

Tottenham italazimika kulipa fidia ya £10m iwapo mkufunzi wa zamani Mauricio Pochettino ataichukua timu nyengine kabla mwisho wa msimu. (Mirror)

Ombi la klabu ya Sheffield United la kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Norway Sander Berge limekataliwa na klabu ya Genk, huku West Ham pia ikimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Mail)

Beki wa Arsenal Shkodran Mustafi, 27, amehusishwa na kuondoka katika klabu hiyo mwisho wa msimu huu lakini mkufunzi wa Gunners Mikel Arteta anaamini anaweza kubadili mchezo wa mchezaji huyo katika klabu hiyo. (Telegraph)

Skrodan Mustafi
Maelezo ya picha, Beki wa Arsenal Skrodan Mustafi kushoto

Bournemouth inafikiria kuwasilisha ombi la beki wa klabu ya Levski Sofia na Iceland Holmar Orn Eyjolfsson, 29. (90 Min)

Charlton huenda ikamsaini nduguye Paul Pogba , Florentin, mwenye umri wa miaka 29 ambaye amekuwa akiichezea klabu hiyo baada ya kuachiliwa na klabu ya Atalanta katika ligi ya MLS. (Sun)

Charlton pia inafikiria kumleta mshambuliaji wa Tottenham na Ireland Troy Parrott, 17, kwa mkopo. (Mail)

Florentin Pogba

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Nduguye Paul Pogba wa man United Florentin Pogba

Everton inakaribia kumsaini kiungo wa kati wa Inter Milan na Uruguay Matias Vecino kwa dau la £17m. (Gazzetta dello Sport)

Manchester United imekataa kumuuza Chris Smalling kwas dau la £25m licha ya ombi kutoka klabu ya Roma , ambapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 yupo katika mkopo wa muda mrefu (Sun)

Kiungo wa kati wa klabu ya AC Milan na mchezaji wa zamani wa Liverpoool na Uhispania mweye umri wa miaka 26 Suso anatarajiwa kujiunga na klabu Sevilla. (Calciomercato)

Manchester United ina matumaini ya kuweka mkataba na kiungo wa kati wa klabu ya Juventus na Ujerumani Emre Can, 26, ambaye pia aliwahi kuichezea klabu ya Liverpool .. (Express)