Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari 'amuangusha' Anthony Joshua

Anthony Joshua akisujudu mebele ya Muhammadu Buhari

Chanzo cha picha, Tolu Ogunlesi

Maelezo ya picha, Anthony Joshua akisujudu mbele ya rais Muhammadu Buhari kama ishara ya heshima

Bondia wa Uingereza Anthony Joshua alionekana akisujudu mbele ya rais wa Nigeria Muhammadu Buhari mjini London.

Joshua ambaye ambaye ana mizizi yake nchini Nigeria pia aliambia umati uliokusanyika kwamba yuko tayari kusimama na Nigeria iwapo atahitajika.

Picha hizo zimetoa hisia tofauti katika mitandao ya kijamii , huku wakosoaji wa Buhari wakikasirika kwamba Joshua hakuzungumzia kuhusu changamoto zinazowakabilia vijana wa Nigeria.

Joshua alisema hivi katika chapisho lake la Instagram: Ni kuhusu utamaduni na heshima kwa viongozi wetu,

Wengine hatahivyo walimpongeza Joshua kwa kukumbatia mizizi yake ya Nigeria na kusujudu mbele ya rais Buhari - ikiwa ni hali ya kitamaduni kuonyesha heshima kwa wakubwa.

Anthony Joshua akipiga picha ya selfie na Muhammadu Buhari

Chanzo cha picha, Tolu Ogunlesi

Maelezo ya picha, Picha za wawili hao zilizua hisia tofuati mitandaoni

Rais BUhari yupo mjini London kwa mkutano wa uwekezaji ambao hufanyika kila mwaka tarehe 20 ya mwezi Januari. Picha za mkutano huo katika mji mkuu wa Uingereza pia zilichapishwa katika mtandao wa Youtube na kitengo cha habari nchini Nigeria.

Mmoja wa wasaidizi wa Buhari , Tolu Ogunlesi alichapisha picha ya mkutano huo katika twitter akiandika: 'AJ!!! akiwa London na rais'.