Fifa Club World Cup: Sababu tano za kutazama michuano hiyo itakayokuwa Qatar

Kinyang'anyiro cha kuwania kombe la klabu bingwa duniani kimeanza Jumatano huku kila mechi ikirushwa hewani moja kwa moja katika BBC.

Bingwa wa kila bara na waandaaji wa michuano hiyo Qatar wanakutana katika siku 10 katika mechi za muondoano ili kuamua ni nani ambaye atatawazwa bingwa wa dunia huku Liverpool ikiingia katika nusu fainali ya mashindano hayo.

Je ni kwa nini unafaa kutazama mechi hizo? BBC inakupatia sababu tano.

Fursa ya kumtazama Gabigol tena.

Huenda hakushangaza ulimwengu akiwa Inter Milan , lakini mshambuliaji wa Flamengo Gabriel Barbosa maarufu kama Gabigol ni muhimu kumtazama.

Iwapo ulitazama fainali ya michuano ya mwezi Novemba ya Copa Libertodores katika BBC 2 moja kwa moja utajua inamaanisha nini.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 ambaye ameshinda mechi tano akiichezea Brazil alifunga magoli mawili katika fainali baada ya Flamengo kutoka goli moja chini na kuishinda River Plate 2-1 na kushinda Copa Libertadores tangu 1981.

Baadaye alipewa kadi nyekundu kwa kuukejeli uamuzi wa refa.

Fursa ya kutazama timu ambazo hujawahi kuzisikia

Je iwapo tutakwambia kuna timu moja katika michuano hiyo ilioshiriki katika kombe la Ufaransa msimu huu kutoka katika eneo lililo umbali wa maili 10,000?.

Hienghene Sport ni timu ya pili nje ya Austria ama New Zealand kushinda kombe la ligi ya Oceania na kufuzu katika michuano ya klabu bingwa duniani.

Waliwashinda wenzao wa Caledonia Magenta katika fainali.

Kuhusu ubora wa michuano hiyo , mfungaji wa magoli mengi Ross Allen - ambaye alifunga magoli 11 akiichezea Wellington - kwa sasa anaichezea klabu ya Guensey katika daraja la nane la ligi ya Uingereza.

Eneo la New Caledonia ni eneo la Ufaransa lililo katika eneo la Pacific - ambalo lilipiga kura ya kutokuwa na uhuru katika kura ya maoni mwaka uliopita - limekuwa mwanachama kamili wa Fifa tangu 2004.

Kutokana na hali yao, washindi wa kombe la Caledonia wanafuzu kushiriki katika kombe la Coupe de France, huku Hienghene Sport ikipoteza katika katika awamu ya kwanza 2013, 2015 na mwezi uliopita.

Kweli Liverpool pia itashirika

Liverpool ina fursa ya kutawazwa mabingwa wa dunia kwa mara ya kwanza.. The Reds licha ya kushinda mataji sita ya Ulaya , hawajashinda fainali ya kombe klabu bora duniani.

Walipoteza taji hilo la International Cup kwa Flamengo mwaka 1981 na baadaye kwa Independente 1984 na kukataa kushiriki 1977 au 1978.

Wameshiriki katika mchuano mmoja wa kombe la klabu bora duniani ikipoteza 1-0 katika fainali kwa Sao Paolo nchini Japan 2005 baada ya kuilaza klabu ya Costa Rica Saprissa 3-0 katika nusu fainali.

Mechi yao ya nusu fainali Alhamisi ijayo- siku moja baada ya timu tofauti ya Liverpool kukabiliana na Aston Villa katika kombe la Carabao nchini Uingereza - inaweza kuwa dhidi ya timu ya Mexico ya Monterrey, ambayo ilishinda ubingwa wa ligi ya Concacaf.

Liverpool baadaye itacheza tena siku ya Jumapili , katika fainali ama kuwania nafasi ya tatu. Kombe la klabu bora duniani limeelekea Ulaya katika misimu yote ya miaka sita iliopita , huku Real Madrid ikishinda fainali tatu zilizopita.

Washindi wake hawafuzu moja kwa moja, hivyobasi Real Madrid hawawezi kutetea taji lao.

Timu ya pekee ya Ulaya kushindwa kushinda taji hilo katika kipindi cha miaka 12 iliopita ni Chelsea mwaka 2012 . Manchester United iliibuka mshindi wa michunao hiyo 2008.

Maandalizi ya kombe la dunia Qatar

Kombe la dunia litachezwa nchini Qatar miaka mitatu kutoka sasa - na pia mwezi Disemba .

Hivyobasi hii ni fursa kuona taifa hilo dogo linaweza kuhimili kuandaa michuano ambapo mashabiki watakuwa wakitoka kutoka kila eneo.