Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 04.09.2019: Eriksen, Willian, Sessegnon, Sane, Wenger

Manchester United ina mpango wa kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, 27, mwezi Januari mwakani kwa bei iliopunguzwa kandarasi yake ikiingia mwaka wa mwisho katika klabu hiyo .(Sun)

United itamenyana na Inter Milan kupata saini ya Eriksen. (Express)

Tottenham inataka kumsaini mchezaji wa Fulham wa chini ya miaka -20 Steven Sessegnon, ambaye ana uwezo wa kucheza safu ya ulinzi na ya kati - mwezi mmoja baada ya kumsaini pacha wake Ryan kwa £25m. (Sun)

Winga wa Chelsear Willian, 31, ananyatiwa na kocha wake wa zamani Maurizio Sarri ambaye sasa ni mkufunzi wa Juventus, wakati kandarasi ya nyota huyo Stamford Bridge ikiingia mwaka wa mwisho . (Express)

Liverpool inamnyatia kipa wa Trabzonspor ambaye bei yake inakadiriwa kuwa £14m- Ugurcan Cakir. Reds walifuatilia mchezaji huyo wa kimataifa wa Uturuki wa miaka 23- wakati wa timu yake ilipotoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Fenerbahce wikendi iliopita. (Mail)

Meneja wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger, ambaye atatimiza miaka 70 mwezi ujao, anataka kurejea katika wadhifa wa usimamizi - miezi 16 baada ya raia huyo wa Ufaransa kuacha kazi kama kocha wa Gunners kwa karibu miaka 22. (Sun)

Liverpool na Chelsea wanapania kumsajili mshambuliaji wa Wigan Athletic wa miaka 17- Muingereza Joe Gelhardt, ambaye ameshirikishwa mara tatu katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo. (Mirror)

Jaribio la Bayern Munich kumsajili winga wa Manchester City Leroy Sane, 23, msimu wa juto limetibuka baada ya kushindwa kufikia masharti ya mshahara wa mchezaji huyo. (Manchester Evening News)

Beki wa kulia wa England Kieran Trippier, 28, amesema kujiunga na Atletico Madrid kutoka Tottenham mwezi Julai ilikua "hatua kubwa". (Diario AS - in Spanish)

Mlinzi wa Manchester United na England Chris Smalling, ambaye awali alijiunga na Roma kwa mkopo huenda akasalia katika klabu hiyo ya Italia zidi ya msimu huu. (Manchester Evening News)

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa akidai kuwa amekataa ofa ya vilabu kadhaa vilivyotaka kumsajili. (mail)

Juventus imewaondoa wachezaji Emre Can, 25,wa wa Ujerumani, mshambuliaji wa zamani wa Croatia Mario Mandzukic, 33, na beki wa Italia Giorgio Chiellini,35, katika kikosi chake cha mwaka wa 2019-20 cha Champions League awamu ya makundi. (Football Italia)

Tetesi Bora Jumanne

Ujumbe mfupi kutoka kwa Lionel Messi huenda ulivuruga mpango wa Barcelona kumsajili tena mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Neymar, 27, kutoka klabu ya Paris St-Germain. (L'Equipe, via Star)

Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi angelifanikiwa kumpata Neymar msimu huu ikiwa dau la kuvunja rekodi la euro milioni 300 sawa (£272m) lingemfikia. (Le Parisien, via Sport)

Vilabu vya Ligi kuu ya Premia huenda vikaungana kushinikiza dirisha la uhamisho wa wachezaji msimu ujao uendane na ule wa Ulaya. (Telegraph)

Winga Marcus Edwards,20, ambaye wakati mmoja alibatizwa jina la 'Messi mdogo' amehama Tottenham. (Sun)

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, 19, yuko radhi kuhamia Manchester United baada kukiri kuwa "angelipendelea" kurejea England. (Mirror)

Mshambuliaji wa Croatia Ante Rebic, 25, amejiunga na AC Milan kwa mkataba wa mkopo wa miaka miwili kutoka Eintracht Frankfurt, huku mshambulizi Andre Silva, 23, akitarajiwa kuchukua nafasi yake . (Gazzetta dello Sport - in Italian)