Charity Shield: Manchester City wailaza Liverpool kuwa mabingwa kupitia penalti

Manchester City ndio mabingwa wa kombe la Charity Sheild baada ya kuwalaza mabingwa wa kombe la mabingwa Ulaya Liverpool kupitia mikawaju ya penalti.

Manchester City ilishinda kombe la Charity Sheild kupitia mikwaju ya penalti baada ya kuilaza Liverpool katika mechi ya kufurahisha mble ya umati mkubwa katika uwanja wa Wembley.

Penalti ya Georginio Wijnaldum iliokolewa na Claudio Bravo huku Gabriel Jesus akifunga penalti ya mwisho.

Mechi hiyo kati ya mabingwa hao wa Uingereza na Ulaya ilikuwa ya msisimuko mkubwa.

Kiungo mshambuliaji wa City Raheem Sterling alifunga goli lake la kwanza dhidi ya klabu yake ya zamani wakati alipopata pasi ya David Silva akiwa karibu na goli.

Chuma cha goli kiligongwa mara mbili katika kipindi kifupi kunako kipindi cha pili huku Sterling akigonga mwamba huo wa goli aliposalia pekee naye Virgil van Dijk akipiga kichwa kilichogonga mwamba kabla ya Joel Matipo kupiga kichwa kufuatia krosi majimaji ya beki huyo wa kati wa Liverpool.

Wakati wote huo Liverpool walionekana kwamba wataibuka washindi huku Salah akipata nafasi tatu za wazi huku kichwa chake kikiokolewa karibu na mstari wa goli na beki Kyle Walker.

Na mechi ikaelekea katika penalti huku City wakifunga penalti zote.

Manchester City ilianza mechi hiyo bila mshambuliaji anayetambulika huku Sterling akicheza kama mbele.

Hali hiyo ilikuwa kwa kipindi cha dakika 13 baada ya jeraha la Leroy Sane kulazimu mabadiliko ambapo Gabriel Jesus aliingia .

Sane hatahivyo alikuwa katika hali nzuri iliomruhusu kupanda ukumbi wa Wembley kuchukua medali yake.

Wakati alipoondoka City ilikuwa inaongoza huku Sterling akifunga wakati ambapo walisalia na wachezaji 10 pekee uwanjani.

Liverpool kujilaumu kwa kukosa nafasi za wazi

Kevin De Bruyne ambaye alikosa kipindi kirefu cha msimu uliopita kupitia majeraha alionyesha umahiri wake hususan katika kipindi cha kwanza huku akihusika pakubwa katika goli la kwanza.

Raia huyo wa Ubelgiji alimpata David Silva ambaye alimpigia pasi Sterling na kufunga.

Kombora lake kali lilimlenga moja kwa moja Allison lakini lilikuwa na kasi na hakuweza kulipangua.

City walizuiliwa baada ya kipindi cha kwanza lakini wangeweza kufunga magoli zaidi huku Sterling akigonga mwamba wa goli naye Jesus akikanyaga pasi iliotolewa na David Silva.

Alitarajiwa kwamba angeonyesha maarifa na kufunga alipopata pasi nyengine muruwa kutoka kwa Walker lakini akajichanganya alipojaribu kumchenga Allison.

Rodri ambaye alikuwa akicheza kama beki mkabaji aliimarika katikati kipindi kirefu cha mchezo.

Lakini alipatikana akiota ndoto mara moja baada ya Salah kumpokonya mpira ,lakini Bravo ambaye alionyesha mchezo wa hali ya juu aliokoa shambulizi lake.