Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 24.07.2019: Rose, Alderweireld, Maguire, Longstaff, Nelson, Lo Celso

Mo Sala na Danny Rose

Chanzo cha picha, Getty Images

Paris St-Germain wameishinda Juventus katika kinyang'anyiro cha kumsaini mlinzi wa Tottenham Danny Rose, 29, na wanaamini watafikia mkataba wa pauni milioni 20 kumsajili kiungo huyo wa kimataifa wa England . (Sun)

Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy, yuko tayari kuongeza bei ya Toby Alderweireld,30 hadi pauni milioni 40 ikiwa mkataba unaodhibiti uhamisho wa mchezaji huyo raia wa Ubelgiji utakufikia kikomo chakaIjumaa hii. (Telegraph)

Naibu mwenyekiti mkuu wa Manchester United, Ed Woodward yuko mbioni kushughulikia suala la usajili wa wachezaji wapya, zikiwa zimesalia wiki mbili kabla ya muda wa mwisho wa uhamisho wa wachezaji kukamilia. (ESPN)

Woodward ana matumaini ya kukamilisha mchakato wa usajili wa mlinzi wa timu ya taifa ya England na klabu ya Leicester City, Harry Maguire, 26, na mchezaji wa safu ya kati wa Newcastle Sean Longstaff, 21. (London Evening Standard)

Harry Maguire

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mlinzi wa England na Leicester City, Harry Maguire

Mkufunzi wa Arsenal Unai Emery ana wiki mbili kuamua ikiwa atamuachilia winga wa England wa chini ya miaka-21 Reiss Nelson, 19, kujiunga na Hertha Berlin kwa mkopo msimu ujao. (Sun)

Mkufunzi wa Celtic Neil Lennon, anatarakiwa kufanya mazungumzo na beki wa Scotland Kieran Tierney, 22, baada ya ofa ya tatu ya Arsenal ya kumnunua mchezaji huyo kukataliwa. (Daily Record)

Tottenham wanakaribia kumsaini kiungo wa kati wa Real Betis Muargentina Giovani lo Celso, 23, kwa kima cha pauni milioni 45. (Sun)

Giovani Lo Celso in action against Real Madrid

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Lo Celso scored 16 goals for Real Betis last season

Mchezaji wa safu ya kati wa Sporting Lisbon na Ureno Bruno Fernandes, 24, amesema kuwa ataendelea kucheza katikaligi kuu ya Ureno licha ya tetesi zinazomhusisha na uhamisho wa kwenda Manchester United. (Mirror)

Sporting na Manchester United bado hawajakubaliana kuhusu bei ya Fernandes. Klabu hiyo ya ligi kuu ya England imesalia na £7m kufikia bei ya kununua nyota huyo wa Ureno anayekadiriwa kuwa £62m. (Star)

Bruno Fernandes

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Bruno Fernandes

Liverpool haitamruhusu kiungo wa kati wa England mwenye umri wa chini ya miaka -21 Ovie Ejaria kuondoka klabu hiyo kwa mkopo msimu huu - lakini wako tayari kumuuza mchezaji huyo. (Liverpool Echo)

Mlinzi wa Manchester City Tosin Adarabioyo, 21, ambaye msimu uliopita alikuwa West Brom kwa mkopo, anajiandaa kujiunga na Blackburn. (Manchester Evening News)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp bado anapania kumnunua mchezaji mwingine mmoja msimu huu. (Liverpool Echo)

Jurgen Klopp celebrates

Chanzo cha picha, Getty Images

Tetesi Bora Jumanne

Barcelona wako tayari kufanya mazungumzo na Lionel Messi, 32, kurefusha mkataba wa nyota huyo raia wa Argentina kwa miaka minne zaidi. (ESPN)

Lionel Messi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Lionel Messi has scored 650 goals in his career for Barcelona and Argentina

Uwezekano wa Real Madrid kumsajili kiungo wa kati wa Manchester United Mfaransa Paul Pogba, 26, utategemea kuondoka kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Wales Gareth Bale, 30, kuondoka klabu hiyo ya Uhispania. (AS)

Bale, ambaye anapokea pauni 550,000 kwa wiki katika uga wa Bernabeu, ambako ana mkataba wa hadi mwaka 2022, anataka marupu rupu yanayolingana na wachezaji wakuu duniani kuondoka Real Madrid, kinasema chanzo cha habari kilicho na uhusiano wa karibu na nyota huyo. (Sky Sports)

wachezaji wa United Paul Pogba (kushoto) na Romelu Lukaku

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Usajili wa Pogba (kushoto) kujiunga United ulivunja rekodi alipohamia klabu hiyo kutoka Juventus mwaka 2016

Toby Alderweireld anatarajia kusalia Tottenham, licha ya Roma kuhusishwa na uhamisho wa mlinzi huyo wa miaka 30 raia wa Ubelgiji ambaye masharti ya mkataba wake yanasema lazima auzwe ikiwa klabu inayotaka kumnunua ina uwezo wa kufikia ada ya pauni milioni 25 kufikia Alhamisi wiki hii. (Telegraph)

Spurs defender Toby Alderweireld

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Toby Alderweireld was tipped for a move away from Spurs in the summer

Arsenal wako mbali sana kufikia kiwango cha pauni milioni 80 zinazoitishwa na Crystal Palace kumwachilia Zaha, huku wasimamizi wa Selhurst Park wakipuuzilia mbali ofa za hivi karibuni za kutaka kumnunua kiungo huyo. (Independent)

Mkufunzi wa zamani wa Chelsea Maurizio Sarri anataka kumjumuisha mlinzi wa Tottenham Danny Rose, 29, katika kikosi chake cha Juventus. (Mail)