Sare mpya ya Manchester City na nyinginezo zilizosisimua katika soka

Manchester City inasema sare yake mpya "inatatiza, inavutia na inathubutu", lakini imezusha mjadala katika mitandao ya kijamii. Tutanatupia jicho jezi nyingine zilizo sisimua katika miaka ya nyuma.

Sergio-Aguero-Raheem-Sterling-and-Leroy-Sane-in-Manchester-Citys-new-3rd-kit.

Chanzo cha picha, Manchester City

Maelezo ya picha, Manchester City inasema sare yake mpya "inatatiza, inavutia na inathubutu". Ina rangi za kuvutia bila ya shaka, baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii wanasema inaonekana kama iliyomwagiliwa kinywaji, wengine wakisema inakaa kama pipi. Je wewe unaionaje?
Nigeria-players-posing-in-Nigeria-kit.

Chanzo cha picha, Fifa/Getty

Maelezo ya picha, Mtu anaweza kuhoji, sare ya Nigeria katika Kombe la dunia mnamo 2018 iliumiza macho. Lakini mashabiki kote duniani waliipenda! Sare hiyo iliuzwa kikamilifu Uingereza muda mfupi baada ya kuchapishwa katika mtandao wa Nike. watu milioni 3 waliiagiza kabla ya kuanza kuuza jambo linalomaanisha kwamba iliwavutia wengi. Huenda inaonyesha kwamba sio mitindo isiyo na mambo mengi ndio huvutia pekee.
Lionel-Messi-and-Xavi.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Hata Lionel Messi, mojawapo ya wanasoka bora duniani hawezi kukwepa vazi lililozusha mjadala. Katika msimu wa 2012-13, Barcelona ilichagua jezi hii ilio mithili ya jua linalochomoza. Je mashabiki wwalilazimika kuvaa miwani ya jua kuwatazama wachezaji wakati wa mechi!
John-Barnes-surrounded-by-Norwich-players-in-a-terrible-kit.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Miaka ya 1990 kulishuhudiwa maajabu uuwanjani na hata nje ya uwanja. Katika iliyofahamika kama 'sare ya kinyesi cha ndege', Norwich City iliitumia sare hii kwa misimu mitatu mtawalia.
Jorge-Campos.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kutana na Jorge Campos - alikuwa kipa wa Mexico na mshambuliaji katika miaka ya 90. lakini sio hilo tu, lakini pia mtindo wake wa mavazi uliwastaajabisha watu. Aliruhusiwa kubuni mtindo wa sare yake ....
Jorge-Campos.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Hili ni mojawapo yavazi alilolibuni mwenyewe. Urefu wake Jorge ulikuwa futi 5 na inchi 6 , na sio urefu wa kawaida kwa kipa, huenda pengine ndio alihitaji nguo zenye rangi kali kutatiza washambuliaji wa timu pinzani . Je unaweza kuivaa hii?
Ryan-Giggs.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mtazame Ryan Giggs kushoto, akiichezea Manchester United katika sare ya kijivu. wachezaji walilaumu jezi hiyo kuchangia mchezo mbaya wa nusu ya kwanza wa mechi dhidi ya Southampton mnamo 1996 na kulazimika kubadilisha katika nusu ya pili. Wachezaji walisema walikuwa hawaonani.
Cameroon-football-team-sleeveless-shirts.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mashati yasio na mikono, Cameroon?! Timu hiyo iliiva sare hii katika mashindanoya kombe la mataifa Afrika mnamo 2002. Fifa liliipia marufuku jezi hiyo katika mashindanoya Kombe la dunia mwaka uo huo.
David-Norton-wearing-hull-tiger-kit.

Chanzo cha picha, PA

Maelezo ya picha, Chui Milia kwa Hull City. Huenda baadhi wakasema pengine timu imeizidi walipozindua sare hii mnamo 1993. Mapenzi kwa wanyama - unaionaje hii?!
Tim-Howard-in-camouflage-kit.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Tim Howard... yuko wapi? Sare mithili ya magwanda ya kijeshi . Mnamo 2011 kipa wa Everton alitinga mtindo huu.
Ruud-Gullit.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Hii nayo ilikuwa ya Chelsea kati ya 1995 na 1996.