Wachezaji wapya waliojiunga na ligi ya Uingereza EPL: Manchester City ,Tottenham, Arsenal, Chelsea , Liverpool na Manchester United

Divock Origi

Chanzo cha picha, Getty Images

Mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi ametia saini kandarasi ya muda mrefu na Liverpool.

Raia huyo wa Ubelgiji, mwenye umri wa miaka 24, alijiunga na Liverpool kutoka Lille 2014 kwa mkataba wa miaka mitano kabla ya kuhudumu misimu miwili kwa mkopo.

Lakini alirudi na matokeo mazuri akifunga mara mbili dhidi ya Barcelona katika nusu fainali ya kombe la mabingwa wa Ulaya kabla ya kufunga goli la ushindi dhidi ya Tottenham katika fainali ya kombe hilo.

''Hisia zangu ni kwamba nilitaka kusalia katika klabu hii . Kuna kitu maalum kinachoendelea hapa''.

Rodri

Chanzo cha picha, Getty Images

Rodri

Manchester City wanakaribia kumsaini mchezaji wa Uhispania Rodri kutoka klabu ya from Atletico Madrid kwa dau litalakovunja rekodi ya klabu hiyo la £62.8m baada ya kulipa ada ya kumuachilia kulingana na timu hiyo ya Uhispania.

Atletico imesema kuwa wakili wa mchezaji huyo na wawakilishi wa City walilipa ada hiyo ya kuwachiliwa kwa mchezaji huyo siku ya Jumatano.

Rodri mwenye umri wa miaka 23 tayari amevunja mktaba wake na Atletico ambao ulitarajiwa kukamilika ,mwezi Juni 2023.

Itaipiku rekodi ya awali ya City ya £60m wakati walipomsaini Riyad Mahrez mwaka 2018.

Rodri alijiunga na Atletico mnamo mwezi Mei 2018 baada ya kuhudumu miaka mitatu katika klabu ya Villarreal na aliichezea kwa,mbau hiyo mara 34.

Tanguy Ndombele

Tottenham imesajili kiungo wa kati wa Ufaransa Tanguy Ndombele kutoka klabu ya Lyon kwa dau lililovunja rekodi la £53.8m .

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ametia saini kandarasi ya hadi 2025 na dau hilo huenda likaongezeka hadi Yuro 70m akiongezewa marupurupu.

Rekodi ya uhamisho ya awali katika timu hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Davinson Sanchez aliyesajiliwa kutoka Ajax kwa dau la £42m.

Tanguy Ndombele

Ndombele alijiunga na Lyon 2017 na kuisaidia kumaliza katika nafasi ya tatu katika ligi ya Ufaransa msimu uliopita.

Pia alicheza mara mbili dhidi ya Manchester City katika mechi za raundi ya muondoani za kombe la mabingwa Ulaya.

Aaron Wan-Bissaka

Wan Bissaka

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester United imemsaini mchezaji wa Uingereza na beki wa kulia wa Crystal Palace Aaron Wan-Bissaka kwa dau la £50m .

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ambaye aliichezea Palace mara ya kwanza mwaka uliopita amekubali kutia saini kandarasi ya miaka mitano ambayo itamfanya kupokea £80,000 kwa wiki.

United tayari imelipa £45m mapema , na kumfanya Wan-Bissaka kuwa mchezaji wa tano aliyesainiwa kwa dau kubwa , baada ya Paul Pogba, Romelu Lukaku, Angel di Maria na Fred.

Man United ilithibitisha usajili wake siku ya Jumamosi

Mkufunzi Ole Gunnar Solskjaer alisema kuwa Wan-Bissaka alikuwa beki bora anayechipuka katika ligi ya Premia.

Gabriel Martinelli

Gabriel Martinelli

Chanzo cha picha, Getty Images

Arsenal imekamilisha uhamisho wa kwanza msimu huu baada ya kumsaini kinda wa Brazil Gabriel Martinelli.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 18 ametia saini kandarasi ya muda mrefu , Arsenal imethibitisha.

Martinelli amejiunga na Arsenal kutoka klabu ya Ituano ambapo alikuwa amefunga magoli 10 katika mechi 34 baada ya kuanza kuichezea klabu hiyo ya Brazil 2017.

''Nataka mchezo wangu kufanana na ule wa Ronaldo'', alisema Martinelli.

Ni mchezaji ambaye anafanya kazi kwa bidii akiweka juhudi za kuafikia malengo yake. Kila mara anapigania kushinda mataji.

Marcus Rashford

Marcus Rashford

Mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford ametia saini makubaliano ya mshahara wa £200,000 kwa wiki ili kusalia katika klabu hiyo hadi mwezi June 2023, akiwa na fursa ya kuongeza mkataba wake kwa mwaka mmoja.

Mshambuliaji huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 21 alijiunga na United akiwa na umri wa miaka saba kabla ya kuanza kukichezea kikosi kikuu cha timu hiyo 2016 akiwa na umri wa miaka 18.

Mateo Kovacic

Mateo Kovacic

Chelsea imemsaini kiungo wa kati wa Croatia Mateo Kovacic kutoka Real Madrid kwa dau la £40m, licha ya kuhudumia marufuku ya miaka miwili.

Kovacic alihudumu misimu miwili iliopita kwa mkopo akiichezea The Blues , akiwasaidia kushinda kombe la Yuropa na anajiunga kwa mkataba wa miaka mitano.

Chelsea tayari iliukuwa imemsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 wakati alipokuwa kwa mkopo hivyobasi hakuhitaji usajili upya.

Marufuku hiyo ya uhamisho iliotolewa na Fifa itahudumu hadi 2020 Januari.

David De Gea

David De Gea

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester United wamemuongezea kipa wa Uhispania David de Gea mashahara katika harakati za kumrai kusalia katika timu hiyo.

Mkataba wa De Gea unakamilika baada ya miezi 12 na juhudi za kumfanya mchezaji huyo kutia saini kandarasi mpya zimegonga mwamba.

Inajulikana kwamba ofa iliotolewa na Man United itamfanya kuwa kipa anayelipwa zaidi dunini.

Karibia ajiunge na Real Madrid 2015.