Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Real Madrid: Wanaweza kumnunua Paul Pogba na kufikia kanuni ya usawa wa malipo?
Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba ametoa ishara wazi kwamba huenda akaondoka Old Trafford, akitaja msimu huu wa joto kama "wakati mzuri wa kuhama kwingine".
Mshindi huyo wa Ufaransa wa Kombe la Dunia amehusishwa na tetesi za kujiunga na miamba wa Uhispania Real Madrid kwa kitita kikubwa na klabu yake ya zamani ya Juventus.
Lakini swali ni je Real wataweza kumnunua nyota huyo wa miaka 26 na kudumisha sheria ya usawa wa kifedha(FFP)?
Kieran Maguire, mtaalamu wa masuala ya kifedha wa kandanda kutoka Chuo Kikuu Liverpool, ananachambua zaidi suala hili.
1. Real wamemnunua nani kufikia sasa ?
Baada ya Thibaut Courtois kujiunga nao kutoka Chelsea last msimu uliopita, Real wamejiepusha na usajli wa majina makubwa kutoka mwaka 2014, wakati Toni Kroos naJames Rodriguez walipotua katika uwanja wa Bernabeu.
Lakini wametumia karibu pauni milioni 300 tangu mwisho wa msimu uliopita - klabu hiyo ilitumia ivunja rekodi ya kwa kutumia kima cha pauni milioni 227 sawa na (euro milioni 254) mwaka 2009 baada ya kuwapata wachezaji wakubwa kama vile Cristiano Ronaldo, Karim Benzema, Kaka na Xabi Alonso.
Mchezaji mwingine mkubwa waliyemsajili ni mshambuliaji wa Ubelgiji Eden Hazard, ambaye alijiunga nao kutoka Chelsea kwa kitita cha fedha zaidi ya pauni milioni 150.
Mshambuliaji wa Serbia Luka Jovic alisajiliwa kutoka Eintracht Frankfurt kwa pauni zunazoripotiwa kuwa milioni 53 na pia walimnunua beki wa kushoto na nyuma Ferland Mendy kutoka Lyon kwa mkataba unaokadiriwa kufikia pauni milioni 47.1.
Mlinzi wa Porto Eder Militao pia alisajiliwa kwa paiuni milioni 42.7 mwezi machi na mshambuliaji wa Brazil Rodrygo, 18, alisainiwa kutoka Santos kwa pauni milioni 40 mwezi Juni mwaka 2018,na amejiunga na kikosi cha real hivi karibuni.
2. Wanaweza kumnunua Pogba?
Uchanganuzi wa mahesabu ya fedha ya Real inaashiria kuwa wana uwezo wa kutumia hela zaidi.
Katika akaunti zao za mwisho zilizotengwa, Real ilikuwa na pato la euro milioni 751, na licha ya wao kuondolewa mapema katika michuano ya Champions League msimu wa 2018-19, walifanikiwa kujikusanyia mapato kutokana na mechi za kirafiki na mauzo ya kibiashara huenda zikafidia pengo lililopo.
Real pia watanufaika ka mabadiliko katika mfumo wa kuhesabu pesa zinazolipwa ya vilabu ambavyo hadi msimu wa mwaka 2018-19 zimekuwa zikifanya vizuri dhidi ya vilabu vingine kwa misimu kumi katika michuano ya Champions League na Europa League.
Japo Real imetumia fedha nyingi msimu huu pia ilijihifadhia euro milioni 100 baada ya kumuuza Ronaldo kwenda Juventus msimu uliopita, ambayo itaingia katika akaunti zao za mwaka 2018-19.
Kwa hivyo klabu hiyo, huenda ikawa na nafasi kiasi ya usajili mpya msimu huu.
3. Watawezaje kusawazisha vitabu vyao?
Uuuzaji wa wachezaji ndio njia rahisi zaidi kwasababu kikosi hicho ni kikubwa kufuatia usajili wao wa msmu uliopita hadi wa leo, lakini faida ya Realkatika miaka ya hivi karibuni inamaanisha kuwa hawana hofu ya ya kuwauza kwa bei ya chini.
Real walikua na jumla ya euro milioni 190m katika benki yao kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa mwzi Juni mwaka 2018.
Fedha zilizotumika msimu huu kufikia sasa zinaweza kuonekana nyingi lakini malipo ya uhamisho wa kisasa hufanyika pole pole.
Ikiwa kikosi hicho kinacho onekana kuna uwezekano wa klabu hiyo ikitaka kuwasaini Gareth Bale na Rodriquez, basi tarajia uhamisho mmoja ua mbili wa wachezaji kwa mkopo ili kuondoa gharama zao kutoka kwa vitabu vya uhasibu vya Real.