Paul Pogba afichua kuwa alikuwa Mecca kuhiji

Chanzo cha picha, Pogba/Instagram
Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba amefikchua kuwa alisherehekea kukamilika kwa mfungo wa mwezi wa Ramadhani kwa hija mjini Mecca.
Mfaransa huyo amefanya ziara hiyo mwishoni mwa Ligi mbili za Primia.
Pogba, ambaye huenda ataondoka Old Trafford msimu huu, aliambatana na mlinzi wa Chelsea Kurt Zouma kwa hija katika mji mtakatifu wa kiislamu.
Pogba amefichua picha zake alizopiga nchini Saudi Arabia, huku zikiwa na maelezo yanayosema : " Kamwe usisahau mambo muhimu katika maisha ".

Chanzo cha picha, Pogba/Instagram
Kiungo huyo wa safu ya kati ya mashambulizi aliwahi kutembelea Mecca kufanya hija - ambayo ni safari ambayo kila muislamu mwenye umri wa utu uzima anatarajiwa kuifanya maishani mwake.
Anatarajiwa kuwa mchezaji wa kwanza wa kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa katika michuano ya kufuzu kwa kombe la Euro 2020 mwezi ujao kabla ya kuchukuliwa kwa uamuzi juu ya klabu yake ya baadae.
Pogba analengwa na meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane, na kiungo huyo wa kati hajaficha kuhusu nia yake ya kuhamia Bernabeu.

Chanzo cha picha, Pogba/Instagram
Taarifa zinasema kuwa malipo ya Pogba yamekuwa kikwazo katika mazungumzo na Real, huku mchezaji huyo wa safu ya kati akitaka malipo ya Euro milioni £13 kwa mwaka.
- Pogba alifanikiwa kunawiri chini ya uongozi wa mpito wa kocha Ole Gunnar Solskjaer lakini kiwango chake cha soka kilishuka mwishoni mwa msimu pamoja na wachezaji wenzake wa manchester United. Uhamisho wa Paul Pogba wachunguzwa na Fifa
Alikosana na mashabiki wakati Manchester United waliposhindwa na Cardiff katika fainali za Championi Ligi , katika mchezo aambao huenda ulikuwa ndio wa mwisho kwake kuonekana uwanjani kama mchezaji wa manchester United.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakati huo huo , mchezaji aliyecheza na Pogba zamani katika klabu ya Juventus Claudio Marchisio amemuomba arejee Turin.
"Niliiangalia timu ya Juventus, nadhani inamkosa mchezaji ambaye anaweza kuisaidia timu kwa kuiongezea nguvu na Pogba anaweza kuwa mchezaji anayefaa kwa hilo ," Marchisio alililiambia gazeti la Tuttosport.
"sijawahi kuelewa huamuzi wake wa kurejea Manchester; alishawahi kuwa huko.
Ni kwa nini aliamua kuwa Muislam?.
Katika majhojiano na waandishi wa habari Paul Pogba alisema kuwa Muislam kumemsaidia kuwa ''mtu bora''

Chanzo cha picha, Pogba/Instagram
katika mahojiano na gazeti la kila siku la Uingereza The Times , Pogba alisema hakulelewa kama Muislamu ,licha ya kwamba mama yake alikuwa ni Muislamu.
Alifichua kuwa alianza 'kujiuliza mwenyewe kuhusu mambo mengi' kabla ya kuwa Muislamu na kuwa mtu mwema 'kuwa mwenye amani ndani'.

Chanzo cha picha, Pogba/Instagram
Pogba alianza kuwa na nia ya kuwa Muislamu baada ya kuamua kufanya utafiti wa dini hiyo na kuwafuata marafiki zake kadhaa kwa kubadili imani na kiungo huyo wa kati wa Man United anasema uamuzi wake ndio uliomsaidia kuwa mtu bora zaidi.
Anakiri kuwa alifanya hivyo ili awe mtu mwenye malengo.
"kusema kweli ni dini ambayo ilinifungua akili na hilo labda linanifanya niwe mtu mwema.Unakuwa na uhusiano na ubinadamu na kuheshimika kwa yule uliye ,dini uliyonayo, rangi gani ya mwili na kila kitu. Uislamu ni - heshima kwa binadamu ".












