New York: Rubani afariki baada ya helikopta kuanguka juu ya jumba la ghorofa 54

Firefighter looks up at the scene

Chanzo cha picha, AFP

Muda wa kusoma: Dakika 3

Rubani mmoja amefariki dunia baada ya kutua ghafla helikopta juu ya jumba la ghorofa 54 mjini Manhattan.

Helikopta hiyo ililipuka na kushika moto ilipogonga kituo cha AXA Equitable, na hakuna majeruhi mengine yalioripotiwa.

Rubani ametambuliwa kama Tim McCormack, huku uchunguzi ukianza kufanywa kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Walioshuhudia ajali hiyo wanasema jumba hilo lilitetemeka ndege ilipoanguka juu yake hali ambayo iliwakumbusha wakazi wengi mashambulio ya kigaidi ya Septemba mwaka 2001.

Maafisa hata hivyo wamefutilia hofu kuwa huenda ajali hiyo ni imetokana na tukio la kigaidi.

Ajali hiyo ilitokea vipi?

Ajali hiyo ilitokea nyakati za mchana wakati wa mchana katika barabara ya 787, kaskazini mwa ukumbi wa Times Square.

Ndege hiyo ya injini mbili chapa Agusta A109E, iliyokuwa na rubani pekee yake, ilikuwa safarini kutoka Manhattan kuelekea uwanja wa ndege wa Linden mjini New Jersey.

Mabaki ya ndege hiyo juu ya paa la ghorofa

Chanzo cha picha, @FDNY

Maelezo ya picha, Mabaki ya ndege hiyo juu ya paa la ghorofa

Lakini dakika 11 baada ya kuanza safari ilianguka juu ya jumba la ghorofa 54, katika kile kinaelezewa kuwa kutua kwa dharura.

Meya wa jiji la New York City Bill de Blasio amesema helikopta hiyo "imeharibiwa kabisa... kutokana na jinsi ilivyogonga chini kwa nguvu".

Maafisa wa kitaifa wa usalama wa angani wanachunguza kwanini helikopta hiyo ambayo ilikuwa katika safari ya hali ya juu iliamua kusafiri wakati wa hali mba ya hewa .

Bw. De Blasio amesema hajali hiyo haikuwa "hali ya kawaida ", na kuongeza kuwa helikopta hiyo ilihitaji kibali maalum kutoka uwanja wa LaGuardia mjini New York City.

Mamlaka ya usimamizi wa angani zinasema kuwa walekezi wao walihindwa kudhibiti ndege hiyo.

Jengo hilo liko nusu maili kutoka Jumba la Trump Tower, na usafiri wa anga katika maeneo hayo umedhibitiwa kwasababu jengo hilo linamilikiwa na Donald Trump ambeye sasa ni rais wa Marekani.

Watu wanasemaje?

Gavana wa jimbo la New York, Andrew Cuomoamesema: "Ikiwa wewe ni mkazi wa New York, bila shaka uliathiriwa na shambulio la kigaidi la Septemba 9/11. Ajali hii imetukumbusha shambulio hilo.

"Kwa hivyo niliposikia helikopta imegonga jengo mawazo yangu yalielekezwa kwa mawazo ya kila makazi wa New York.''

map showing where AXA Equitable building is
Presentational white space

Rais Trump amesema ajali hiyo ni "mkasa mkubwa" na ni tukio la ''kusikitisha".

Nicolas Estevez mmoja wa watu walioshuhudia ajali hiyo aliliambia shirika la habari la Reuters: kuwa "nilisikia mlipuko na mosho mkubwa ukifuka" hali iliyomkumbush shambulio la Semptemba 2011 (9/11).

Kipande cha chuma cha ukibwa wa (30cm) kilianguka barazani mita chache kutoka hapa, alisema

Michaela Dudley, wa Hoboken, New Jersey, ambaye anafanya kazi katika jengo hilo , anasema alihisi kama ni "matetemeko madogo ya ardhi".

Mabaki ya ndege hiyo juu ya jumba la ghorofa

Chanzo cha picha, New York City Fire Department

Maelezo ya picha, Mabaki ya ndege hiyo juu ya jumba la ghorofa

"Nilianza kusikia milio ya magari ya zima moto na hapo nikajua kitu kibaya kimetokea,"alisema wakili huyo wa miaka 30.

"Kulikua na tangazo la kutuagiza tutoke ndani ya jengo hilo. Na bila kupoteza wakati nilifungasha virago vyangu , nikachukua simu na kutoka. Eneo la ngazi lilikua limejaa watu waliokua waking'ang'ana kutoka. Tulikua na wasiwasi kwasababu hatukua na ufahamu ni nini kimetokea na watu walikuwa wamejawa na hofu."

Rubabui alikua nani?

Tim McCormack alitajwa kuwa mtu mwenye ujuzi mkubwa na rubani mkongwa ambaye pia alikuwa afisa wazima moto wa kujitolea.

Shirika la habari la ABC lilitangaza taarifa iliyokua imetolewa na familia ya McCormack, iliyosema: "Familia yetu leo imempoteza mtu wa maana sana, leo ndugu yetu amefariki dunia akifanya kazi aliyoipenda na kutekeleza kwa uadilifu mkubwa.

Ilisema kuwa alitua ghafla juu ya baa la ghorofa "ili asisababishe maafa ya watu wengine bali yake mwenyewe. Ndugu yangu alikuwa shujaa".

Baadhi ya vyombo vya habari nchini Marekani vimeripoti kuwa Bw. McCormack aliwahi kutua helikopta salama baada ya ndege kukwama ndani ya injini mwaka 2014.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Presentational white space