Ndege yaanguka katika paa la nyumba Marekani
Ndege hii ilijipata imekwama katika paa la nyumba baada ya kuanguka mjini Connecticut.
La kushangaza ni kwamba rubani wa ndege hiyo alijipata na majeraha madogo.
Vyombo vya habari vinasema alipatikana katika dari ya nyumba hiyo akitafuta miwani yake.
Alitarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa Manispaa ya Danbury yapata kilomita 4.5 kutoka nyumba hiyo wakati betri ya ndege hiyo ilipofeli.