Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 03.03.2019: Carrick, Benitez, Sancho, Bale, Eriksen, Caballero, Almiron

Jadon Sancho

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Jadon Sancho(kushoto)

Manchester United inakabiliwa na kinyang'anyiro kikali kutoka kwa Paris St-Germain katika usajili wa winga wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 18. (Mirror)

Real Madrid iko tayari kutoa mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 29, ili ifanikiwe kumsaini kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, 27. (Mirror)

Manchester United itapewa mshambuliaji wa Argentina Mauro Icardi, 26, huku Inter Milan ikimlenga mshambuliaji wa Ubelgiji, Romelu Lukaku, 25, katika mkataba wa kubadilishana wachezaji. (Express)

Romelu Lukaku

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Romelu Lukaku

West Ham inajiandaa kumsajili kiungo wa kati wa England Jonjo Shelvey, 27, kutoka Newcastle msimu ujao wa joto. (Sun)

Mmiliki wa Newcastle United Mike Ashley ameghairi mpango wa kuuza klabu hiyo baada ya kukosa mnunuzi wa kisawa sawa tangu alipotangaza kuuza klabu hiyo miezi 17 iliyopita. (Times - subscription required)

Meneja wa New Leicester Brendan Rodgers amemwambia mshambuliaji wa England Jamie Vardy, 32, kwamba anamtegemea sana katika juhudi zake za kuimarisha timu hiyo. (Telegraph)

Jamie Vardy

Chanzo cha picha, Rex Features

Maelezo ya picha, Jamie Vardy

Mchezaji nyota wa Manchester City, Bernardo Silva atapewa mkataba mpya wa miaka sita. (Mail)

Manchester City italazimika kujitahadhari na AC Milan na Juventus ikiwa ina azma ya kumsajili winga wa Dinamo Zagreb, Antonio Marin, 18. (Calciomercato)

Chelsea inatarajiwa kumuongezea kipa wake Muargentina Willy Caballero, 37, mkataba wa mwaka mmoja. (Sun)

Willy Caballero

Chanzo cha picha, BBC

Maelezo ya picha, Willy Caballero

Manchester United itaipatia Benfica ofa ya euro milioni 180 sawa na pauni (£155m) kuwasaini Ruben Dias, 21, na Joao Felix, 19. (Record - in Portuguese)

Shirikisho la soka duniani Fifa inapania kupinga mpango wa Chelsea wa kutumia euro milioni 200 kuwasajili wachezaji wapya kabla marufuku ya usajili dhidi yao kuanza kutekelezwa.

Mpango huo ukiidhinishwa huenda ukaathiri mpango wa Chelsea wa kumsajili Zinedine Zidane kama meneja wao mpya. (Sun)

Zinedine Zidane

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Zinedine Zidane(Kulia)

Manchester City itatumia euro milioni 350 msimu huu wa joto kuimarisha kikosi chake huku meneja Pep Guardiola akiwa na mpangowa kuwasajili wachezaji wanne wa ziada. (Star)

Guardiola analenga wachezaji kutoka klabu yake ya zamani ya Bayern Munich - kuna tetesi huenda akamsaini kiungo wa kati wa Uhispania Thiago Alcantara, 27. (Mirror)

Juventus hunda ikasaini meneja wa zamani wa Chelsea, Antonio Conte ikiwa Massimiliano Allegri atawaondokea miamba hao wa ligi ya Serie A msimu huu. (Corriere Dello Sport - in Italian)

Antonio Conte

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Antonio Conte

Juventus Pia wanawalenga mameneja wa Manchester City Pep Guardiola na Liverpool Jurgen Klopp. (Tuttosport - in Italian)

Mlinzi wa Manchester United na Sweden Victor Lindelof, 24, anasema kuwa aliwaenzi sana kipa wa zamani wa United na UfaransaFabian Barthez alipokuwa akicheza mpira akiwa mdogo japo wakati huo alikuwa akicheza namba 10. (Mail)

Tetesi Bora Jumamosi

Real Madrid itaangalia utaratibu wa kumuuza mshambuliaji Gareth Bale,29,kipindi cha majira ya joto (AS in Spanish)

Gareth Bale

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Gareth Bale

Inahofiwa huenda mshambuliaji wa Tottenham Hary Kane akaondoa klabuni hapo kama timu hiyo itaendelea kuwa na ukame wa kutwaa mataji(Telegraph)

Chelsea wako kwenye mazungumzo na mshambuliaji Eden Hazard. (Le10Sport in French)

Arsenal wanajianda kumsajili kinda wa miaka 17 wa Brazil Gabriel Martinelli kwa dau la pauni Milioni 4. (Goal via Mirror)

Wakati huo huo The Gunner ni moja ya klabu inayowania saini ya beki wa kushoto wa Ajax na Argentina Nicolas Tagliafico(ESPN