Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 01.12.2018: Fabregas, Barbosa, Christensen, De Gea, Collins
Kiungo mshambuliaji wa Chelsea Cesc Fabreagas amesema ataendelea kusalia Chelsea mpaka mwisho wa mkataba wake ingawa mhispania huyo anavivutia vilabu vingi kwenye dirisha dogo la Januari. (Talksport)
AC Milan ipo katika mazungumzo ya kumsajili mlinzi wa Chelsea Christensen pamoja na kiungo mshambuliaji Cesc Fabregas,32. (Gazzetta dello Sport - in Italian)
Klabu ya Barcelona imewaweka kwenye mipango ya kuwasajili mlinzi wa Manchester city Vincent Kompany, 32, na Msebia Branislav Ivanovich,34, katika kumaliza changamoto za ulinzi katika timu hiyo mwezi januari. (Mirror)
Klabu ya Chelsea inakutana na ugumu wa kumshawishi mshambuliaji wa kiingereza Callum Hudson Odoi kusaini mkataba mpya kutokana na kinda huyo kuhitaji kuhakikishiwa kucheza katika kikosi cha kwanza. (Guardian)
Real Madrid imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa haimuachii kinda wake Brahim Diaz,19 kwenda Manchester city. (As-in Spanish)
Inter Milan iko tayari kumtoa kwa mkopo mshambuliaji wa Kibrazil, Gabriel Barbosa ambaye yuko Santos kwa mkopo kwa dau la pauni 18 ambapo vilabu vya Everton, west ham na crystal palace vinavutiwa kumnunua mpachika mabao huyo.(Mail)
Mchezaji wa zamani wa Manchester united Zlatan Ibrahimovic 37 alikataa kusajiliwa Manchester city miaka nane iliyopita baada ya Kocha Pep Guardiola kutaka kumuuza walipokuwa Barcelona. (Sun)
Klabu ya Chelsea imekataa kumwachia mlinzi wake Andres Christensen 22, kwenda Barcelona. (Mirror)
Wakala wa Mlinda mlango Divid De Gea wa Manchester united Jorge mendes amethibitisha kuwa David ataongeza mkataba mpya katika klabu hiyo kuendelea kusalia. (Star)
Winga wa Croatia Ivan Perisic amesema alikuwa mbioni kujiunga na Manchester united akitokea Inter Milan (FourFourTwo)
Mlinzi wa zamani wa west ham James Collins ,35, amekubali kusaini mkataba Wa miaka mitano katika klabu ya Aston Villa(Mail)
Beki wa Wolves Matt Doherty amesema wamiliki wa klabu hiyo wanafikiria kushinda ubingwa wa EPL ndani ya miaka sita ijayo ambapo wamepanga msimu huu kuishia nafasi ya 10 za juu. (Express and Star)
Baba wa mshambuliaji wa Everton Richarlison amebashiri mwanake atakuwa mfungaji bora wa kombe la dunia mwaka 2022. (Liverpool Echo)
Kiungo wa Kijerumani na klabu ya Brighton Pascal Gross,27, ametarajia kupiga hatua kubwa kwa jadon Sancho na wachezaji wengine kwenda ujerumani.
Kikosi cha Manchester United kimesafiri kwa ndege Southampton ingawa kwa kuchelewa baada ya matatizo ya kiusafiri yaliyotokea. (Mail)