Tetesi za soka Ulaya Jumatano: Messi, De Gea, Ake, De Ligt, Alonso

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United itaipatia umuhimu kandarasi mpya ya kipa wa Uhispania David de Gea, 27, baada ya kupiga hatua kubwa katika mashauriano ya kurefusha mikataba ya beki wa kushoto wa England Luke Shaw, 23, na mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 22. (Evening Standard)
Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi huenda akapewa idhibati ya kuondoka klabu hiyo bila malipo ifikapo mwaka 2020, endapo mchezaji huyo wa miaka 31- raia wa Argentina hatajiunga na ligi nyingine kubwa. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Chanzo cha picha, Getty Images
Tottenham inafuatilia kwa karibu mchezo wa mlinzi wa Bournemouth na Uholanzi Nathan Ake, 23. (Sky Sports)
Spurs inamtaka beki wa kati wa Sampdoria raia wa Denmark Joachim Andersen,22. (Sport Mediaset - in Italian)
Barcelona pia inapania kumsajili mlinzi wa kati wa Ajax mwenye umri wa miaka 19 Matthijs de Ligt kama chaguo lao kuu. (Marca)
Beki wa kushoto wa Uhispania Marcos Alonso, 27, amesema kuwa anajiandaa kutia saini kandarasi ya kurefusha muda wake katika klabu ya Chelsea "siku chache zijazo". (AS, via Evening Standard)

Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal imeungana na AC Milan na Inter katika Kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo wa kati wa Cagliari na Italia Nicolo Barella, 21. (Gazzetta dello Sport - in Italian)
Galatasaray na Besiktas watamenyana kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi mwezi Januari, japo Everton pia imeonyesha azma yake ya kumsajili kiungo huyo wa Ubelgiji wa miaka 23. (Turkish Football, via Talksport)
Bournemouth inapanga kufanya mazungumza na winga wa Uskochi Ryan Fraser, 24. (Sun)
Newcastle United inakaribia kufikia mkataba mpya na kiungo wa kati wa Uingereza Sean Longstaff, 20. (Chronicle)

Chanzo cha picha, SNS
Manchester City inatilia shaka hali ya uwanja wa Wembley watakapochuana na Tottenham Jumatatu ya Oktoba , 29 , huku uga huo ikitarajiwa kuandaa mechi NFL siku moja kabla yao. (Manchester Evening News)
Meneja wa zamani wa England Sam Allardyce anasema kiungo wa kati wa Tottenham naThree Lions Eric Dier, 24, ni mzuri sawa na mwenzake wa Barcelona na Uhispania Sergio Busquets, 30. (Talksport)
Na Kiungo wa kati wa zamani wa Arsenal Robert Pires amesema kuwa an a uhakika "100%" kwamba klabu hiyi itamaliza liga ya primia katika nafasi ya nne bora mzimu huu. (Express)














