Tetesi za soka Ulaya:Messi, De Gea, Shaw, Bale, Butland, Foden, Ramsey, Sarr, Havertz

Chanzo cha picha, Getty Images
Timu ya Manchester United ina mpango wa kumuongezea mkataba wa David de Gea kwa lazima miezi sita mapema kwa kutumia kifungu kilicho kwenye mkataba wake wa sasa, kama goli kipa wa Spain hataafikiana mkataba mpya na klabu hiyo kabla ya mwezi Januari. (Sun)
Mshambuliaji wa Wales,Gareth Bale, 29 amejipanga kukabiliana na juhudi zozote zile za Real Madrid kutaka kumlazimisha ahamie Manchester United majira mwishoni mwa msimu huu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Juventus inaweza kumtaka kiungo wa Arsenal na Wales Aaron Ramsey, 27, kama watashindwa kumpata kiungo wa Ufaransa anayechezea Paris St-Germain Adrien Rabiot, 23. (Express)

Kuna taarifa kuwa Manchester City walitaka kumlipa mara tatu zaidi ya kiwango anacholipwa kwa sasa mchezaji nyota wa Barcelona na Argentina Lionel Messi, 31, kama angekubali kusaini mkataba nao. (Mundo Deportivo kupitia Sun)
Messi anaweza kuondoka Barcelona mwaka 2020 lakini mkataba wake unaeleza kuwa kama ataondoka basi hataruhusiwa kujiunga na timu nyingine "kubwa". (Mundo Deportivo)

Chanzo cha picha, Reuters
Bingwa wa soka kutoka Argentina Diego Maradona amedai kuwa Messi sio kiongozi kwa sababu huwa anaenda maliwatoni mara 20 kabla ya mechi kuanza.(La Ultima Palabra kupitia Standard)
Antonio Valencia anakaribia kuihama Manchester United bila malipo yoyote kutokana na kifungu kilichopo kwenye mkataba wake. Mchezaji huyo Ecuador anaweza kusaini mkataba mpya katika klabu nyingine kuanzia mwanzo wa mwezi machi. (Sun)
Imeripotiwa kuwa Real Madrid kwa sasa wanapatia kipaumbele ununuzi wa mkabaji wa kati kwa ajili ya msimu ujao. (Marca)
Golikipa wa Stoke na England Jack Butland, 25 anataka kujiunga na wakala aliyemuongoza Wayne Rooney katika maisha yake ya uchezaji, katika juhudi zake za kutaka kurejea katika Ligi ya Premia.
Manchester United wanadaiwa kuwasilisha ofa ya euro milioni 60 kumtaka mchezaji Nikola Milenkovic ,21 wa Fiorentina na Serbia. (La Nazione via Metro)
Chelsea imempa kiungo wa Ufaransa N'Golo Kante, 27, mkataba mpya katika juhudi za kutaka kuhakikisha anasalia Stamford Bridge huku akiendelea kutafutwa na Paris St-Germain. (Mirror)
Chelsea, Tottenham na Liverpool watalazimika kulipa euro 60 kama watataka kusaini mkataba na Krzysztof Piatek, 23 ambaye ni mchezaji wa Genoa na Poland. (Football.London)

Chanzo cha picha, PA
Tottenham imempa mkataba mpya kiungo wa Denmark Christian Eriksen, 26, ili asalie nao huku taarifa zikidokeza kwamba Real Madrid wanataka kumnunua (Mundo Deportivo)
Manchester United inatafuta ushrikiano na klabu ndogo ya Uhuspania itakayosaidia kujenga vipaji vya wachezaji wa Man U ilikuzuia matatizo yanayoweza kuchipuka wakati Uingereza itajiondoa kutoka muungano wa Ulaya.(Marca via Mirror)
Rais wa ligi ya Uhispania ,La Liga , Javier Tebas wanawataka Menweja wa Manchester City Pep Guardiola na Mwenzake wa Manchester United Jose Mourinho kurudi katika ligi hiyo.(Mail)
Meneja wa Napoli Carlo Ancelotti ambae alikuwa Kocha wa zamani wa Chelsea ametunukiwa na kampuni ya kuoka Pizza mjini Naples, kwa kutengeneza mlo wa Pizza uliona sura ya Meneja huyo. (Gazzetta dello Sport via 90min)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa zamani wa Crystal Palace Shaun Derry ameseme itapendeza zaidi ikiwa klabu hicho kitamsajili mchezaji kiungo wa Chelsea na England Ruben Loftus-Cheek, mwenye umri wa 22. (Love Sport Radio via Football.London)
Mmiliki wa wa Timu ya Bolton Ken Anderson amefichua kuwa amepokea mapendekezo kutoka kwa wawekezaji wa kutoka nje ya kununua klabu hicho kwa £30m. (Bolton News)












