Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 21.09.2018: Maier, De Jong, Barella, Knockaert, Zaha

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United na Arsenal wanammezea mate kiungo wa kati wa kikosi cha chini ya miaka 21 wa Hertha Berlin mwenye umri wa miaka 19 Arne Maier. (Sport Bild)
United pia wamejiunga na Tottengam kumg'ang'ania kiungo wa kati wa Ajax Frenkie de Jong. Maajenti walitumwa kumtazama mchezaji huyo mwenye miaka 22 raia wa Uholanzi akicheza dhidi ya Ufaransa mapema mwezi huu. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Liverpool wamepata msukakumo wanapoendelea na mikakati ya kumwinda kiungo wa kati wa Cagliari Nicolo Barella, 21, baada ya Juventus kujitoa kutoka mbio za kumsaka raia huyo wa Italia wa kikosi cha chini ya miaka 21. (Calciomercato)
Raul Sanllehi - mkuu mpya wa kandanda huko Arsenal ana matumaini ya kumuunganisha kiungo wa kati wa Sevilla Ever Banega, 30, na meneja Unai Emery huko Emirates. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Sanllehi pia anammezea mate mshambuliaji mwenye miaka 22 wa Boca Juniors raia wa Argentina Cristian Pavon. (football.london)
Jurgeni alibadilisha sera za Liverpool za kununua wachezaji kutoka "wingi kwenda ubora" wakati akimtafuta Virgil van Dijk kutoka Southampton. (FourFourTwo)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwandishi wa habari Mhispania Guillem Balague anasema mchezaji wa Barcelona raia wa Argentina Lionel Messi, 31, na mwenye miaka 33 wa Juventus raia wa Ureno Cristiano Ronaldo wana mambo mengi pamoja (BBC Radio 5 live Football Daily)
Aliyekuwa mchezaji raia wa Italia Francesco Totti anasema alijaribu kuwashawishi Ronaldo na mshambualiaji raia wa Sweden Zlatan Ibrahimovic, 36, kujiunga naye huko Roma wakati wa siku zake za kucheza. (La Repubblica, via Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images
Wing'a wa Crystal Palace Wilfried Zaha anaserma alikuwa "ahera" wakati wa kipindi chake huko Manchester United. Mechezaji huyo raia wa Ivory Coast alicheza mara mbili wakatia wa kipindi cha miaka mwili akiwa Old Trafford. (Shortlist)
Mlinzi wa zamani wa West Ham James Collins, 35 amealikwa kufanya mazoezi na Aston Villa, wakati meneja Steve Bruce anatarajiwa kumasaini mchezaji huyo asiye na ajenti (Telegraph)

Chanzo cha picha, Getty Images
Swansea wanatarajiwa kumuongezea mkataba aliyekuwa mchezaji wa kikosi cha chini ya miaka 21 raia wa England Matt Grimes. (Sun)
Bora Kutoka Alhamisi
Kiungo wa kati wa Chelsea raia wa Brazil Willian, 30, anasema hakuwa na mpango wa kuondoka stamford Bridge msimu huu licha ya vilabu vya Manchester United na Barcelona kuonyesha dalili ya kumsaini. (Express)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa England Marcus Rashford, 20, anapata mafunzo zaidi kutoka kwa mchezaji mwenzake wa Manchester United Romelu Lukaku.
Meneja wa England Gareth Southgate amemtuma naibu wake Steve Holland kumtazama Jack Grealish wakati wa ushindi wa Aston Villa dhidi ya Rotherham siku ya Jumanne wakati anafikiria kumsaini kiungo huyo wa kati wa umri wa miaka 23. (Birmingham Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa Juventus na Ureno Cristiano Ronaldo, 33, anasema itakuwa vigumu kwa mtoto wake wa umri wa miaka nane ambaye pia anaitwa Cristiano kucheza mpira kama yeye. Ronaldo Junior anaichezea Juventus Academy. (BeIn Sports, via Sun)
Totttenham wametupilia mbali madai kuwa uwanja wao mpya hautakuwa tayari ifakapo mwanzo wa mwaka 2019. (Sky Sports)
Mkuu mpya wa kandanda huko Arsenal Raul Sanllehi, anataka kumsaini wing'a raia wa Argentina Cristian Pavon, 22, kutoka Boca Juniors. (Football London)












