Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uefa kuanzisha michuano mingine mipya ya soka
Shirikisho la soka barani Uefa linatarajia kuazisha michuano mingine mipya na ya tatu kwa ukubwa soka barani humo baada ya ile ya klabu bingwa ulaya na Europa ligi.
Kwa Mujibu wa wa mwenyekiti wa Muungano wa vilabu barani ulaya, Andrea Agnelli, michuano ya hiyo ya tatu kwa ukubwa inatarajiwa kuanza kuanzia mwaka 2021.
Agnelli amesema michuano itasaidia kuongeza vilabu vinavyoshirikia michezo ya ulaya utoka 80 mpaka 96
Hata hivyo katibu huyo wa muungano wa vilabu hakufafanua muundo upi utatumika katika michuano hiyo mipya.
Wazo la kuanza kwa michuano hiyo kutaifanya michuano ya Europa ligi kupungua timu toka timu 48 mpaka 32. Hivyo michuano yote itakuwa na idadi sawa ya timu.