Siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho Ulaya: Wachezaji 7 maarufu wanaotarajiwa kujiunga na klabu mpya

Chanzo cha picha, Getty Images
Dirisha la uhamisho la klabu za Uingereza tayari limefungwa lakini BBC michezo inaangazia makubaiano ambayo huenda yakakamilishwa barani Ulaya
Timu zilizopo nje ya Uingereza zinaweza kufanya makubaliano ya uhamisho hadi saa moja usiku saa za Afrika mashariki , huku madirisha ya uhamisho ya Uhispania, Ujerumani na Ufaransa pia yakifungwa siku ya leo.
BBC Michezo inaangazia baadhi ya wachezaji wa Ulaya ambao huenda wakamia klabu mpya.
Ivan Rakitic (Barcelona)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kuwasili kwa Arturo Vidal na Arthur kunatoa ushindani mkubwa kwa Ivan rakitric katika safu ya kati ya klabu ya Barcelona.
Huku hatma ya mchezaji wa Ufaransa Adrien Rabiot ikiwa haijulikani katika klabu ya Paris St-Germain, klabu hiyo ya Ligue 1 inamnyatia kiungo huyo wa kati wa Croatia na wanataka kuimarisha kitita cha uhamisho wake cha £112m
Jerome Boateng (Bayern Munich)

Chanzo cha picha, Getty Images
Uwezekano wa beki huyo wa Ujerumani Boateng kusalia na mabingwa hao wa Bundesliga uko nusu nusu
Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City alihusishwa na uhamisho wa Manchester United msimu huu , lakini klabi hiyo ya ligi ya dara la kwanza huenda ndiko anakoelekea.
Shinji Kagawa (Borussia Dortmund)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa zamani katika klabu ya Manchester United Kagawa hakushiriki katika mechi ya ufunguzi wa klabu ya Dortmund dhidi ya RB Leipzig na ameripotiwa kutokuwa miongoni mwa mipango ya meneja mpyaLucien Favre
Huku mchezaji mpya aliyesajiliwa Axel Witsel na Thomas Delaney wakitarajiwa , mchezaji huyo wa Japan huenda akaondoka katiika uwanja wa Westfalenstadion katika siku ya mwisho ya uhamisho.
Claudio Marchisio (Free agent)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kandarasi ya kiungo wa kati wa Itali Marchisio katika klabu ya Juventus ilikatizwa kutokana na makubaliano kati ya pande zote mbili na sasa anatafuta klabu mpya.
Porto na Benfica wamehusishwa ijapokuwa klabu nchini Ureno zina hadi tarehe 21 Septemba kufanikisha makubaliano yao.
Lazar Markovic (Liverpool)

Chanzo cha picha, Getty Images
Ni kweli kwamba bado ni mchezaji wa Liverpool. Raia huyo wa Serbia alijiunga na Liverpool kwa dau la £20m kutoka benfica 2014, lakini hajaichezea klabu hiyo tangu 2015.
Ruben Loftus-Cheek (Chelsea)

Chanzo cha picha, Getty Images
Loftus-Cheek alihudumu msimu uliopita kwa mkopo katika klabu ya Crystal Palace, ambapo mchezo wake ulimfanya kuitwa katika kikosicha cha timu ya taifa ya Uingereza cha kombe la dunia.
Huku Jorginho, N'Golo Kante, Ross Barkley na Mateo Kovacic wakiwa mbele yake katika wachezaji wanaotarajiwa kucheza katika kikosi vcha kwanza cha timu katika klabu ya Stamford Bridge, Loftus-Cheek huenda akaanza kutafuta klabu mpya.
Mario Hermoso (Espanyol)

Chanzo cha picha, Getty Images
Real Madrid huenda ikaanza kumtafuta kiungo wa kati anayetumia mguu wa kushoto iwapo Jesus Vallejo na Hermoso watalengwa
Hermoso alijiunga na Espanyol kwa dau la £360,000 msimu uliopita na Real ina fursa ya kumnunua tena mchezaji huyo kwa dau la £13.5m.












