Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 31.08.2018 Lookman, Fekir, Bony, Modric, Choupo-Moting

Chanzo cha picha, Getty Images
Everton ina imani itaendelea kumshikilia Ademola Lookman, licha ya klabu ya RB Leipzig, kuvutiwa na winga huyo wa England ambao wako tayari kulipa £ milioni 25 kwa mchezaji huyo mwenye miaka 20. (Liverpool Echo)
Chelsea ilikataa nafasi ya kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Lyon na timu ya taifa ya Ufaransa Nabil Fekir, mwenye umri wa miaka 25, katika msimu wa joto. Kwa mujibu wa rais wa klabu hiyo ya Ufaransa Jean-Michel Aulas. Fekir alilengwa na timu ya Liverpool. (Mail)
Mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain wanatumai kukamilisha mkataba wa mshambuliaji wa miaka 29 kutoka Stoke City na timu ya taifa ya Cameroon Eric Maxim Choupo-Moting. (Mail)
Timu katika ligi ya Ujerumani Bundesliga - Hoffenheim wanamlenga mchezaji wa miaka 18 wa Arsenal Reiss Nelson kwa mkopo msimu mzima. (Metro)
Strasbourg na Lazio zinataka kumsajili mchezaji wa PSG kutoka Marekani Timothy Weah, 18, kwa mkopo. (L'Equipe)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mchezaji kutoka Ivory Coast Wilfried Bony, mwenye umri wa miaka 29, huenda anakaribia kuhamia Galatasary kutoka Swansea City wakati mkuu wa Swans Graham Potter akitazamia kupunguza matumizi ya klabu hiyo kwa kumuondea mchezaji huyo.(WalesOnline)
Huku Bony akihusishwa na uhamisho kwenda ng'ambo, mchezaji wa kiungo cha mbele wa Real Madrid raia wa Uhispania Dani Gomez, huenda akaijunga na klabu hiyo bingwa kwa mkopo. (WalesOnline)
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Croatia Luka Modric, mwenye umri wa miaka 32, anasema anataka kusalia Real Madrid "kwa miaka mingi ijayo," huku rais wa klabu hiyo Florentino Perez akisema Inter Milan haitaki "kulipa chochote" katika kumsajili mchezaji huyo mapema msimu wa joto. (Football Italia)
Winga wa Liverpool raia wa Serbia Lazar Markovic, mwenye umri wa miaka 24, anatarajiwa kukamilisha uhamisho wa mkopo kuelekea upande wa Ugiriki PAOK. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images
Bosi wa West Ham Manuel Pellegrini anasema alikataa nafasi ya kumsajili aliyekuwa mchezaji wa Manchester City Yaya Toure, mwenye umri wa miaka 35. (Talksport)
Aston Villa inatarajiwa kumsajili mlinzi rai awa Ufaransa Harold Moukoudi, mwenye miaka 20, kwa mkopo kutoka kwa Le Havre kabla ya kufikiwa mkataba wa thamani ya £ milioni 10 mwezi Januari. (Mirror)
Blackburn haitomruhusu Bradley Dack, mwenye umri wa miaka 24, kuondoka kwenye klabu hiyo baada ya kuktaa ombi lenye thamani ya ziada ya £ milioni 5 kwa mchezaji huyo wa West Brom. (Sky Sports)

Aliyekuwa mshambuliaji wa Brazil Ronaldo atanunua rasmi kalbu katika ligi ya Uhispania Real Valladolid Jumatatu. (AS - in Spanish)
Beki wa kulia wa England Danny Simpson, mwenye umri wa miaka 31, na mchezaji wa kiungo cha kati wa Wales Andy King, 29, wanatarajiwa kuondoka Leicester kabla ya muda wa mwisho leo Ijumaa wa uhamisho wa kimataifa.(Leicester Mercury)
Aliyekuwa mchezaji wa kiungo cha kati wa England Gareth Barry, aliye na miaka 37, atakuwa na jukumu kuu kwa West Brom msimu huu kwa mujibu wa meneja Darren Moore. (Express and Star)












