Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 20.08.2018 Karius, Stones, De Gea, Loftus-Cheek, Robertson
Kipa wa Liverpool Loris Karius, 25, anafanya mazungumzo na Besiktas, huku mkuu wa Reds Jurgen Klopp akiridhia kuondoka kwa Mjerumani huyo. (Mirror)
Manchester City inataka kuongeza mkataba wa mlinzi wa England John Stones wenye thamani ya £120,000 kwa wiki. Mkataba wa mchezaji huyo kwa sasa unaendelea hadi 2022. (Sun)
Kipa wa Uhispania David De Gea, mwenye umri wa miaka 27, anakaribia kusaini mkataba mpya wa thamani ya £200,000 kwa wiki na Manchester United. (Mirror)
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Chelsea Ruben Loftus-Cheek, mwenye miaka 22, atazungumza na maafisa wa klabu wiki hii kuhusu mustakabali wake. Mchezaji huyo wa kimataifa ataomba kuhamishwa kwa mkopo iwapo meneja Maurizio Sarri hatoweza kumhakikishia muda atakaoichezea timu hiyo. (Sun)
Beki wa Scotland Andrew Robertson hana haraka ya kusaini mkataba mpya Liverpool; na huenda hakutokuwa na majadiliano msimu huu kuhusu mkataba mpya wa mchezaji huyo wa miaka 24.(Liverpool Echo)
Leon Bailey - anayelengwa na Manchester United, Liverpool na Chelsea - amesaini mkataba mpya huko Bayer Leverkusen. Mshambuliaji huyo mwenye miaka 21 raia wa Jamaica alihusishwa na uhamisho katika msimu wa joto. (Goal)
Tazama pia:
Mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya Uhispania Alvaro Morata, 25, anasema "hapakuwa na fikra yoyote" kwamba angeondoka msimu huu, licha ya uvumi kuhusu mustakabali wake. (Mail)
Bosi wa Tottenham Mauricio Pochettino amesema "amechoshwa" na kujadili uhamisho. (Sky Sports)
Arsenal haijapiga hatua katika mkataba mpya wa mchezaji wa kiungo cha kati Aaron Ramsey, mwenye miaka 27, ambaye mkataba wake unamalizika msimu ujao wa joto. (Sun)
Aston Villa inatafakari kumwania winga wa Liverpool Sheyi Ojo, huku timu ya Liverpool ikiwa na hamu kubwa kumuachia kwa mkopo mchezaji huyo wa England timu ya wachezajiw asiozidi miaka 21. (Birmingham Live)
Mshambuliaji wa Liverpool na Ubelgiji Divock Origi analengwa na Borussia Dortmund, lakini timu hiyo ya Ujerumani haijawasilisha ombi rasmi kwa mchezaji huyo wa miaka 23.(Liverpool Echo)
Liverpool imekuwa ikitumia mifuko ya mpira wa raga kumtayarisha kipa wa Brazil Alisson Becker kwa kibarua kigumu katika ligi ya England.(Telegraph)
Bora zaidi kutoka Jumapili
Kiungo wa Wolves Mreno Ruben Neves mwenye miaka 21 ameingia kwenye rada za Manchester City na klabu hiyo inataka kumsajili mchezaji huyo katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari kwa dau la pauni milioni 60(Sun on Sunday)
Klabu ya Barcelona imekubali kuwa timu ya Manchester United haitomuuza kiungo wake Mfaransa Paul Pogba, kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili tarehe 31, mwezi huu, ila wataangalia uwezekano wa kumsajili mchezaji huyo dirisha lijalo la usajili . (Sunday Express)
Bosi wa zamani wa vilabu vya Everton, Manchester United, Sunderland na West Ham David Moyes anaongoza mbio za kupewa nafasi ya kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Marekani (Sunday Times - subscription only
Manchester City wameambiwa watalazimika kuilipa Borussia Dortmund's kiasi cha pauni milioni 68, kama inataka kumsajili kiungo Julian Weigl, ambae pia anawindwa na miamba ya soka ya Ufaransa Paris St-Germain (France Football, via Sun on Sunday)
Chelsea iko tayari kusikiliza ofa itayokuja klabuni hapo ikimtaka mchezaji wa kiungo Danny Drinkwater, ambae ameanza katika michezo mitano tu ya msimu uliopita akiwa amesajiliwa kwa kiasi cha pauni 35 akitokea Leicester City (Mail on Sunday)
Meneja wa Newcastle, Rafael Benitez anawaniwa na klabu ya Tianjin Quanjian,ya nchini china inayoshiriki katika ligi ya nchi hiyo (Sunday Mirror)