Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 15.08.2018: Zidane, Pogba, Messi, Godin, Rose, Herrera, Cattermole, Odegaard, Grujic

Zinedine Zidane

Chanzo cha picha, Getty Images

Mkufunzi wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane anataka kurudi katika kazi yake ya ukufunzi na anajiandaa kumrithi Jose Mourinho katika klabu ya Manchester United msimu ujao. (L'Equipe - in French)

Mkurugenzi wa Barcelona Ariedo Braida anasema klabu yake haiwezi kutoa ofa kwa Paul Pogba wa Manchester United msimu huu, lakini amemtaja mchezaji huyo Mfaransa mwenye miaka 25 kama mchezaji mzuri na atakuwa anamfuatilia Mfaransa huyo. (Mirror)

pogba

Chanzo cha picha, Getty Images

Klabu ya Bundesliga ya Schalke wana mpango wa kutoa mikataba ya kudumu na hawana nia ya kuwasaini beki wa Tottenham raia wa England Danny Rose, 28, au kiungo wa kati wa England Ruben Loftus-Cheek, 22, kwa mkopo. (Sky Sports)

Danny Rose

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Danny Rose

Meneja mpya wa Chelsea Maurizio Sarri amelegeza sheria kali kuhusu lishe na ratiba za mechi zilizowekwa na mtangulizi wake Antonio Conte. (Telegraph)

Sarri yuko radhi kiungo wa kati wa Chelsea mwenye miaka 28 Danny Drinkwater auzwe mwezi huu. (Star)

Lionel Messi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Lionel Messi

Lionel Messi hatacheza kwenye mechi yoyote ya Argentina na haijulikani iwapo mshambuliaji huyo wa Barcelona mwenye miaka 31 atacheza tena mechi za kimataifa. (Clarin)

Mlinzi wa Leicester mwenye miaka 25 Harry Maguire yuko karibu kukubaliana na mkataba wa pauni 75,000 kwa wiki kwenye klabu huyo. (Telegraph)

Patrick Roberts

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Patrick Roberts

Wing'a wa Manchester City mwenye miaka 21 raia wa England Patrick Roberts anatarajiwa kujiunga na klabu ya Uhispania ya Girona kwa mkopo. (Sky Sports)

Meneja wa Arsenal Unai Emery atalazimika kufuata matumizi finyu ya fedha kwenye klabu msimu ujao kwa kununua wachezaji. (Telegraph)

Uwanja mpya wa Tottenham hatakuwa tayari ifikapo Novemba na klabu hiyo itakuwa ikichezea mechi zake zote za nyumbani huko Wembley. (Times - subscription required)

Diego Godin

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Diego Godin

Mlinzi wa Atletico Madrid raia wa Uruguay Diego Godin, 32, alikataa ofa ya kuhamia Manchester United kutokana na sababu za kibinfasi. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Manchester United Ander Herrera, 29, anasema anataka kujitokeza kuichezea klabu hiyo ya Old Trafford baada ya kukamilika kwa mkataba wake msimu ujao. (Mirror)

Marko Grujic

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Marko Grujic

Kiungo wa kati wa Liverpool raia wa Serbia Marko Grujic, 22, huenda akajiunga na klabu ya kigeni kwa mkopo baada ya kukataa ofa kutoka Cardiff City na Middlesbrough. (Evening Standard)

Aliyekuwa meneja wa Bordeaux na Sunderland Gus Poyet yuko kwenye mazungumzo na Black Cats kuhusu kumsaini kiungo wa kati mwenye miaka 30 raia wa England Lee Cattermole on loan. (Guardian)

Martin Odegaard

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Martin Odegaard

Klabu ya uholanzi ya Vitesse Arnhem ina mpango wa kumsaini kiungo wa kati wa Real Madrid mwenye miaka 19 raia wa Norway Martin Odegaard kwa mkopo. (De Gelderlander - in Dutch)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho angependa mlinzi raia wa Argentina Marcos Rojo na mkabaji kamili Matteo Darmian, 28 kusalia kwenye klabu hadi Januari. (ESPN)

Ryan Sessegnon

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ryan Sessegnon

Ryan Sessegnon anasema uvumi kuwa anaondoka Fulham haujakuwa kizungumkuti, na malengo yake sasa ni kucheza na klabu hiyo ya Ligi ya Premio. Mchezaji huyo wing'a mweye miaka 18 amehusishwa na kuhama kwenda Tottenham Hotspur. (Sky

Saint-Etienne wamefikia makubaliano ya pauni milioni 4.4 na Marseille kumsaini aliyekuwa mchezaji wa Newcastle raia wa Ufaransa Remy Cabella, 28. (L'Equipe - in French)

Bora zaidi kutoka Jumanne

Paris St-Germain wanaandaa pauni milioni 100 kwa ofa ya mchezaji wa Tottenham mwenye miaka 26 raia wa Denmark Christian Eriksen. (Express)

Schalke wana nia ya kumasaini mchezaji mwenye miaka 22 raia wa England Reuben Loftus-Cheek kwa mkopo lakini Chelsea haunda wasiruhusu kuondoka kwake. (Telegraph)

Matteo Darmian

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Matteo Darmian

Beki wa Manchester United Matteo Darmian anataka kuondoka Old Trafford na Juventus, Napoli na Internazionale wanamwinda mchezaji huyo mwenye miaka 28 raia wa Italia. (Manchester Evening News)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho alichanganyikiwa kufuatia madai ya Paul Pogba ya kuwepo uhusiano mbaya kati yao siku ya Ijumaa. (Telegraph)

Marcus Bettinelli

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Marcus Bettinelli

Kipa Marcus Bettinelli, 26, anaweza akaamua kuondoka Fulham baada ya kuachwa nje ya kikosi kilichocheza mechi ya kwanza ya msimu. (Mail)

Liverpool watasikiliza ofa kwa mchezaji wa maiaka 32 mlinzi raia wa Estonia Ragnar Klavan. (Liverpool Echo)

Lee Cattermole

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Lee Cattermole

Kiungo wa kati wa Sunderland mwenye miaka 30 Lee Cattermole huenda akahamia Bordeaux, ambapo aliyekuwa meneja wa zamani wa Black Cats sasa ndiye meneja. (Teamtalk)

Wale wanaolengwa kuchukua nafasi ya mkurugenzi mpya wa Manchester United ni pamoja na kipa Edwin van der Sar, mkurugenzi wa Juventus Fabio Paratici na Monchi, mkurugenzi wa zamaniawa Sevilla na sasa Roma. (Independent)

Mshambuliaji Wilfried Zaha anasema bado anazungumza na Crystal Palace kuhusu kuongezwa mkataba wake huko Selhurst Park. (Mail)