Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ligi ya Premia: Uhamisho mkubwa wa wachezaji maarufu ambao haukufanikiwa
Sio vibaya kukubali, Kabla ya msimu uliokwisha kuanza , Mohammed Sala hakujulikana na timu uipendayo , je ni kweli?
Alvaro Morata na Alexandare Lacazette walikuwa miongoni mwa wachezaji waliobeba matumaini ya wengi sio? Ni sawa. Hakuna kati yetu anaweza kutabiri hali ya siku zijazo.
Mara nyengine hata wakufunzi wazuri hukataa uhamisho ambao mara nyengine wanasalia wakijilaumu , ama mara nynegine mambo huenda mrama. Hii hapa ni baadhi ya mifano ambayo huenda ingebadili historia ya ligi ya Uingereza.
Kaka kuelekea Manchester City
Mwaka 2009, kikosi kipya cha Manchester City kilikuwa kikitaka kutumia kitita kikubwa cha fedha kumsajili mchezaji wa Brazil Kaka.
Klabu ya AC Milan na Kaka walivutiwa na dau la City la £108m walilowasilisha .Kilikuwa kitita cha juu zaidi ambapo miaka 10 baadaye kilipitwa na uhamisho wa Neymar na Kylian Mbappe kuelekea klabu ya PSG pekee.
Shabiki mmoja wa City alikuwa ana uhakika kwamba makubaliano hayo yatafanyika na hivyobsi akaweka tatoo ya mchezaji huyo katika kifua chake.
Lakini mwishowe, mshindi huyo wa taji la Ballon d'Or 2007 aliamua kwamba haukuwa wakati mzuri na kukataa fursa hiyo ya kujiunga na Manchester City na hivyobasi kumwacha afisa mkuu wa City akiwa amekasirika na kusema kuwa AC Milan imemkosea.
Steven Gerrard kuelekea Chelsea
Mwaka 2005, baada ya kushinda kombe la vilabu bingwa Ulaya, Steven Gerrard aliwashangaza wengi katika uwanja wa Anfield kwa kuwasilisha ombi la uhamisho.
Mkufunzi mpya kwa jina Mourinho alikuwa ana hamu ya kumsajili mchezaji huyo kwa mradi wake wa Stamford Bridge.
Kulikuwa na hisia kali na tisheti zikachomwa , lakini baadaye kama Jammie Caragher anavyosema , Gerrard aligundua kwamba kuridhika na taji moja akiwa Anfield ni zaidi ya kushinda mataji matatu ama manne Stamford Bridge.
Bahati mbaya kwa wachezaji wote wawili ni kwamba Chelsea imeshinda mataji manne ya ligi ya Uingereza huku Liverpool ikisubiri.
Robert Lewandowski kuelekea Blackburn
Kabla apate umaarufu kama mmojawapo wa washambuliaji bora duniani, Kijana Robert Lewandowsky alikuwa mpango wa mkufunzi Sam Allardyce katika klabu ya Blackburn Rovers .
Klabu hiyo ya Lancashire iliwasilisha ombi la £4m kwa mchezaji huyo wa Poland mwaka 2010.
Hatahivyo majivu ya Volcano yaliweka wingu jeusi angani Iceland na kukatiza usafiri wa ndege na kumzuia Lewandowsky kusafiri kuelekea Blackburn.
Kufikia sasa amekiri kwamba Rovers ilikuwa timu yake ya pili alioipenda baada ya Borussia Dortmund , lakini pengine wikendi moja na Big Sam ingemshawishi kusalia.
Rivaldo kuelekea Bolton Wanderers
Mwaka 2014, Bolton Wanderers walikuwa na ufanisi mkubwa wakiwa ndoto ya kucheza Ulaya.
Sam Allardyce aligonga vichwa vya habari alipoulizia uwezo wa mshambuliaji wa Brazil Rivaldo, 32 ambaye alikuwa akiichezea AC Milan.
Rivaldo alitoa taarifa iliosema: Nataka changamoto ya kutaka kuifikisha Bolton katika michuano ya Ulaya kwa mara ya kwanza katika historia yake, ni wakati mzuri.
Mwishowe, alikuwa na mabadiliko ya kimawazo na kwenda Olympiakos.
Bolton ilimaliza msimu huo ikiwa sawa kwa pointi na Liverpool , ikiwa pointi tatu nyuma ya viongozi wanne wa ligi.
Msimu uliopita walifunga bao la dakika za lala salama katika mechi yao ya mwisho kuzuia kushushwa daraja.
Andriy Shevchenko kuelekea West Ham
Harry Redknapp karibu amsajili mmojawapo wa washambuliaji wazuri zaidi duniani wakati huo akiwa West Ham 1994.
Harry anakumbuka kwamba alikuwa na Shevchenko akimchunguza kwa siku nne katika kikosi cha pili cha Barnet.
Hatahivyo uzoefu wake wa kusajili wachezaji kutoka mashariki mwa Ulaya kulimfanya kumwacha Sheva.
''Hakungo'a miti lakini alikuwa na nidhamu ya kutosha''.
''Lakini huo ni wakati ambapo nilikuwa na matatizo na wachezaji kutoka Romania na nikafikiria kwamba kitu cha mwisho ningetaka ni kumsajili raia wa Ukrain''.
Na ni kupitia maamuzi kama hayo ambapo mchezaji wa haiba ya Sheva aliponyoka.
Zlatan Ibrahimovic kuelekea Arsenal
Mwaka 2000, Arsene Wenger alimwalika kinda raia wa Sweden Zlatan Ibrahimovic kukutana na kikosi chake cha wachezaji kilichojaa vijana.
Alimpatia tisheti iliokuwa na nambari tisa mgongoni na kila kitu.
Kila kitu kilikuwa kikiendelea vizuri hadi pale Wenger alipomwambia kufanya majaribio. Na kama Zlatan alivyoelezea: ''hapana Zlatan harajibiwi''.
Fikiria timu hiyo ikiwa na Zlatan, lo!