Ligi ya Premia: Njia tano za kuwazuia Manchester City msimu wa 2018-19

Chanzo cha picha, Getty Images
Klabu kumi na tisa zilijaribu kuizuia Manchester City kushinda mechi Ligi kuu ya England msimu uliopita. Sita tu zilifaninkiwa.
Mwaka 2017-2018 City walipata pointi nyingi zaidi kuliko timu yoyote ile na kuandikisha ushindi mara nyingi na kufunga mabao mengi kuliko timu yoyote katika ligi kuu ya England iliyowatangulia.
Katika maandalizi ya msimu wa 2018-19 mabingwa hao walitumia pauni milioni 70 kumsaini mchezaji bora wa Ligi mwaka ya 2015-16 Riyad Mahrez.
Hizi ni mbinu ambazo timu zote 19 zinazoweza kutumiwa na timu 19 kuikabili Manchester City.
Cheza vile wanacheza na uwazidi
City wanajua kudhibiti mpira uwanjani na wana kasi ya juu, ni rahisi kuvutiwa na mchezo wao lakini ni vigumu kucheza kama wao.
Lakini wachezaji waliopangwa vizuri wanaweza kuleta matokeo mazuri jinsi Liverpool walivyoonyesha wakati kikosi cha Guardiola kilipata pigo mikononi mwao.

Chanzo cha picha, BBC Sport
Liverpool waliweza kucheza vizuri kutokana na nguvu na kujituma kwao katika safu ya kati na uwezo walio nao kwenye safu ya mbele, ambapo wana washambuliaji stadi wa kutamaniwa na klabu nyingine Ulaya.
Walichodhihirisha Liverpool - jambo ambalo pia walilionyesha katika mechi yao ya kwanza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya hatua ya robo fainali dhidi ya City, na walivyofanya pia Manchester United dakika 16 za kipindi cha pili mara nyingine pekee ambapo City walishindwa msimu huo - ni udhaifu ambao huwezesha klabu kuwafungwa na kuwaumiza zaidi baada ya kuwafunga bao la kwanza.
Hasa Vincent Kompany anapokuwa hayuko uwanjani, kama alivyofanya katika mechi nyingi msimu uliopita kutokana na jeraha.
'Egesha basi'
Hii ndiyo mbinu ambayo timu nyingi zilijaribu kutumia msimu uliopita wakiwa tayari wanafahamu udhaifu walio nao kwa City.
Kutokana na hilo vijana wa Guardiola walitawala mechi hadi asilimia 71.94.
Umiliki huu wa mpira ulikuwa nguzo kuu ya ushindi wa Man City. Lakini timu kadhaa ndogo zilikuwa na uwezo wa kukaidi hilo na mfano ni Burnley na Crystal Palace
Kuzuia mipira
Idadi kubwa ya mabao ya City yalitoka sehemu za uwanja zinazojulikana kama "maeneo nusu wazi" (yanayoelezwa hapa chini)
Kuwanyima wachezaji kama Kevin de Bruyne and David Silva nafasi katika sehemu hizi nje ya kisanduku na kufuatilia mikimbio ya Raheem Sterling na Leroy Sane ni mbinu nyingine muhimu katika kuwazuia City.

Chanzo cha picha, BBC Sport
Liverpool walitumia mbinu hii tarehe 14 Januari, wakinufaika kutoka na kukosekana kwa Silva lakini pia kumnyima De Bruyne nafasi yake ya kawaida mchezoni.
Sane na Sterling pia walinyimwa fursa ya kuingia eneo la hatari jambo ambalo lilifaa baadhi ya timu zilizojimudu dhidi ya City.

Chanzo cha picha, BBC Sport
Tumia mipira ya juu au mbinu ya kujimbu mashambulizi
City walifungwa magoli 27 kwenye ligu msimu uliopita. Lakini kati ya hayo 10 yalitokana na pasi za mipira ya juu au krosi katika eneo la hatari, jambo linaloashiria udhaifu wa City katika mipira ya juu, au kutomakinika zaidi kwa walinzi wake eneo la hatari, au mambo yote mawili.

Chanzo cha picha, BBC Sport
Mbinu za City za kusukuma na kuwapeleka wachezaji mbele inaweza kuwaweka kwenye hatari ya kushambuliwa ghafla.
Newcastle walitumia mbinu hii walipowashinda 3-1 huko Etihad kwa kupata mpira na kuucheza kwa kasi na kwa haraka.
Wigan nao walitumia mbinu kama hii kurusha City nje ya kombe la FA.
Kuwa na bahati
Kuwepo kwa kikosi kilicho bora cha City na usimamizi mwema ina maana kuwa timu nyingi zinahitaji bahati kuweza kupata matokeo mazuri dhidi yao.
Manchester United walijikwamua Etihad lakini hawangefanikiwa iwapo Raheem Sterling, Bernardo Silva au Ilkay Gundogan hawangepoteza nafasi nne za wazi walizokuwa wamepata kwenye mechi hiyo.
Huddersfield nao walifaidi kutokana na kiwango cha chini zaidi cha ufasaha wa City kwenye makombora yao ya kulenga goli kilichoshuhudiwa msimu wote, jambo lililowawezesha kupata sare ya 0-0.
Kuna hali ya kutamauka katika hili, lakini baadhi ya timu zinaweza zikafanikiwa.












