Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Saido Berahino: Mshambuliaji wa Stoke City aruhusiwa na Fifa kuichezea Burundi
Mshambuliaji wa klabu ya Stoke City nchini Uingereza Saido Berahino ataitwa na timu ya taifa ya Burundi baada ya shirikisho la soka duniani Fifa kumpatia ruhusa kulichezea taifa hilo alikozaliwa.
Mshambuliaji huyo ambaye hajafunga bao hata moja katika kipindi cha miezi 29 , ataliwakilisha taifa hilo la mashariki mwa Afrika baada ya kucheza viwango tofauti vya timu ya vijana ya Uingereza.
Berahino mwenye umri wa miaka 24 alichezea kila umri katika timu ya Uingereza kuanzia umri wa miaka 16 hadi 21 kati ya 2009 na 2015.
Aliwachezea mara 47 simba hao wadogo akifunga mara 24, kabla ya kupata wito kuichezea timu kuu mwezi Novemba 2014 katika michuano ya Yuro 2016, mechi dhidi ya Slovenia na mechi ya kirafiki dhidi ya Scotland.
Lakini kwa sababu hakucheza katika mecho zote ,ana uwezo wa kuichezea Burundi ambao mara ya kwanza waliulizia uwepo wake mwezi machi 2015.
Sasa yuko tayari kucheza mechi yake ya kwanza ya kufuzu dhidi ya Gabon katika mechi ya kombe la bara Afrika mwezi ujao baada ya shirikisho la soka nchini Burundi FA kutangaza habari hizo katika mtandao wa twitter.
Mwaka 2013, wakati alipocheza katika kikosi cha West Brom , Berahino alisema: Nataka kucheza katika kiwango cha juu pamoja na wachezaji wenye viwango vya juu katika mashindano makubwa. Burundi ndio taifa ninalotoka. Nitakuwa Mburundi licha ya kitakachotokea, hata iwapo nitakuwa mchezaji wa ligi ya Uingereza niliyefanikiwa pakubwa. Bado nina utamaduni wa Burundi ndani yangu. Ninapoichezea Uingereza ni swala tofauti kwa jumla. Wamenipatia fursa ya pili katika maisha, na kuipatia familia yangu ,maisha tofauti. Natooa shukrani zangu za dhati kwa kile Uingereza walichonifanyia mimi na familia yangu , hivyobasi ninapoichezea Uingereza ninacheza kwa furaha na kuwa na lengo la kushinda.