Afrika nje ya Kombe la Dunia

Senegal wakiondoka uwanjani

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Senegal wakiondoka uwanjani

Ni Kombe la Dunia, lakini kwa Afrika, bara litakuwa bila mwakilishi huku wenzao wakiendelea na safari ya kusaka ubingwa wa Kombe hilo.

Kabla ya ngarambe hizi, nafasi 5 zilizotengewa Afrika zilijazwa na:

  • MISRI
  • MOROCCO
  • TUNISIA
  • NIGERIA
  • SENEGAL

Lakini ni machungu kwa bara hili kwani matumaini ya mwisho, Senegal, imeliaga Kombe baada ya kutapatapa dhidi ya Colombia.

Juhudi za Senegal zinastahili kupongezwa kwani wawakilishi wengine wa Afrika walifunga virago mechi yao ya pili.

Mbali na Nigeria, Senegal ndiye mwakilishi mwingine wa Afrika kusajili ushindi mechi hatua ya makundi.

Kuanzia Jumamosi ijayo, timu 16 zitakuwa viwanja tofauti Urusi kusaka tiketi ya robo fainali. Timu 16 zitakazogusa ngarambe za muondoano zimethibitishwa:

Uruguay, Urusi, Uhispania,

Portugal, Ufaransa, Denmark,

Croatia, Argentina, Sweden,

Mexico, Brazil, Uswizi

Colombia, Japan, Ubelgiji na Uingereza.

Hata hivyo, miujiza si haba Kombe hili kwani mabingwa watetezi, Ujerumani tayari wametemwa baada ya kucharazwa 2-0 na Korea Kusini.

Kila taifa Afrika sasa lina majukumu ya kujiandaa kwa Qatar 2022 kwani wote wana nafasi sawa ya kufuzu!